Naivasha
Naivasha ni mji wa soko katika Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki, nchini Kenya. Umelala kaskazini magharibi kwa Nairobi, kwenye mwambao wa Ziwa Naivasha na kando ya njia kuu ya Nairobi-Nakuru kupinduka na Reli ya Uganda.
Naivasha ni sehemu ya Kaunti ya Nakuru. Mji una idadi ya wakazi wa 181,966 (sensa ya mwaka 2009). [1]
Sekta kuu ni kilimo, hasa upanzi wa maua.
Naivasha pia ni maarufu kama kituo cha utalii. Hifadhi za Hell's Gate na Mlima Longonot ni vivutio vya karibu. Ziwa Naivasha hutembelewa na watalii wanaotazama viboko au kutembea kwenye mbuga wa binafsi wa Crescent Island ndani ya ziwa. [2]
Tangu miaka ya 1990 maeneo makubwa kando ya ziwa yameona upanuzi wa mashamba ya maua yanayolimwa hapa kwa soko la Ulaya.
Mwaka 2004/2005 Naivasha ilikuwa mahali pa mikutano kati ya wawakilishi wa maadui katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Sudan na mapatano ya "Comprehensive Peace Agreement" inajulikana pia kama "Mapatano ya Naivasha".
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]- Kimo = 2,085m
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Sensa ya Kenya 2009, VOLUME IC Population Distribution by Age, Sex and Administrative Units Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, iliangaliwa Januari 2019
- ↑ "Ziwa Naivasha Country Club"(wanyamapori,map,picha), Go2Africa, 2003, go2africa.com webpage: Nav 2003, go2africa.com webpage: Nav.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]0°43′12.85″S 36°25′42.71″E / 0.7202361°S 36.4285306°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Naivasha kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |