[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kisumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kisumu, Kenya


Kisumu
Kisumu is located in Kenya
Kisumu
Kisumu

Mahali pa mji wa Kisumu katika Kenya

Majiranukta: 0°6′0″S 34°45′0″E / 0.10000°S 34.75000°E / -0.10000; 34.75000
Nchi Bendera ya Kenya Kenya
Kaunti
Kisumu
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 968,909
Kitovu cha Kisumu

Kisumu ni mji mkubwa wa tatu wa Kenya, ukiwa na wakazi 968,909 (sensa ya mwaka 2009[1]). Pia ni mji mkubwa wa Kenya ya Magharibi na makao makuu ya kaunti ya Kisumu.

Mji uko kando ya ziwa Viktoria Nyanza, una bandari kubwa ya nchi katika ziwa hilo. Mji na bandari vilianzishwa kwa jina la "Port Florence" mwaka 1901 wakati reli ya Uganda ilipofika huko kutoka Mombasa.

Kuna feri ziwani kutoka Kisumu kwenda Mwanza, Bukoba, Entebbe, Port Bell na Jinja.

Kiuchumi Kisumu ina viwanda kadhaa, hasa vya sukari, samaki, vitambaa, pia ya bia.

Maendeleo ya Kisumu yalikwama miaka mingi kwa sababu kwa miaka mingi Wajaluo walisimama upande wa upinzani wa kisiasa, hivyo serikali haikupeleka miradi tena katika eneo hilo.

Tazama pia

Tanbihi

  1. Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.