Kaunti ya Busia
Mandhari
Kaunti ya Busia ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 893,681 katika eneo la km2 1,696.3, msongamano ukiwa hivyo wa watu 527 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Busia.
Shughuli kuu ya kiuchumi ni biashara na nchi jirani ya Uganda, pamoja na mji wa Busia kituo cha mpakani.
Mbali na mji, uchumi wa wilaya hutegemea sana uvuvi na kilimo, mazao msingi yakiwa pamoja na mihogo, mtama, viazi vitamu, maharagwe, na mahindi.
Wilaya ya Busia ni makao ya kabila la Waluhya nchini Kenya ambao wanapatikana hasa katika sehemu za Magharibi mwa Kenya.
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Kaunti ya Busia ina maeneo bunge saba yafuatayo[2]:
Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3]
[hariri | hariri chanzo]- Bunyala 85,977
- Busia 142,408
- Butula 140,334
- Nambale 111,636
- Samia 107,176
- Teso North 138,034
- Teso South 168,116
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya mito ya kaunti ya Busia
- Busia, Kenya
- Busia, Uganda
- Wilaya ya Busia, Kenya
- Wilaya ya Busia, Uganda
- Wilaya ya Teso
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ http://countytrak.infotrakresearch.com/Busia-county/
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ramani ya Wilaya ya Busia Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
0°26′N 34°9′E / 0.433°N 34.150°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Busia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |