[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Viunganishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mifano
  • Alifyeka lakini hakulima
  • Habiba aliondoka pamoja na mama yake
  • Wao ni binadamu kama sisi
  • Kiache hicho.
  • Kaka na Dada

Viunganishi ni neno au kikundi cha maneno chenye kuunganisha vipashio vya lugha ili kuunda kipashio kikubwa zaidi. Pia ni maneno yanayounganisha maneno mengine. Kiunganishi kinaweza kuunganisha neno na neno, kirai na kirai, kishazi na kishazi, sentensi na sentensi au vinginevyo.

Uchambuzi

[hariri | hariri chanzo]
Mifano ya jumla
  • Baba na mama
  • Analima bila kupanda
  • Baba analima na baba anapanda
  • Shoka limeshindwa sembuse panga

Maumbo ya viunganishi

[hariri | hariri chanzo]

Viunganishi havina maneno ya kupambikwa katika neno au katika kupatanishwa kisarufi ndani ya tungo. Yaani, mfano cheza, chezewa, chezeka, na kadhalika. Hayo ni maumbo ya maneno ambayo hayabadiliki.

Mfano

Na, lakini, ingawa, bila, au, ila, sembuse, kwa sababu, kwa kuwa, pamoja na, ijapokuwa, tena, iwapo, labda, toka, n.k.

Aina za viunganishi

[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina mbili za viunganishi - navyo ni:

Ama:

Viunganishi huru ni vile vinavyosimama pekee katika tungo/katikati ya vipashio vinavyoungwa. Kwa mfano: Sisi tunaimba na kucheza.

Viunganishi tegemezi ni vile ambavyo huunda kwa viambishi vya o-rejeshi vinavyowekwa katika kishazi huru kwa pamoja huunda sentensi changamano. Viambishi hivyo ni kama vile: po, ye, lo, cho n.k. Kwa mfano: Mama anayepika ni msusi.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Viunganishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.