[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kishazi huru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kishazi huru (alama yake ni: K/Hr) ni tungo inayotawaliwa na kitenzi kinachojitosheleza kimaana. Yaani, ni tungo inayotawaliwa na kitenzi kinachotoa taarifa kamili. Kitenzi hicho kinaweza kuwa:

(A) Kitenzi kikuu (T)

Mfano:

  • Watoto wanacheza mpira
  • Mwalimu anaandika darasani
  • Mama anapika chakula jikoni
  • Wanafunzi wanasoma vitabu
(B) Kitenzi kisaidizi + kitenzi kikuu (TS+(-)+T)

Mfano:

  • Watoto walikuwa wanacheza mpira (watoto = nomino ya kawaida, walikuwa = kitenzi kikuu kisadizi, wanacheza = kitenzi kikuu, mpira = nomino ya kawaida).
  • Mwalimu alikuwa anataka kuandika ubaoni (mwalimu = nomino ya kawaida, alikuwa = TS, anaka = TS, kuandika = T, ubaoni = kielezi cha mahali).
  • Mama alikuwa anataka kwenda kununua samaki (mama = N, alikuwa = TS, anataka = TS, kwenda = TS, kununua = T, samaki = T)
Angalizo

Katika mabano juu kuna TS+(-)+T, yaani, hivi TS = kitenzi kisaidizi, (-) = kipashio cha hiari. Kwanini kiwe cha hiari? Tazama hii: "mama alikuwa anataka kwenda kununua samaki". Neno au kirai "kwenda" si lazima kiwepo ndiyo maana ya hiari. Hata kama ingewekuwa: "mama alikuwa anataka kununua samaki" ingeeleweka tu.

(C) Kitenzi kishirikishi (t)

Mfano:

  • Wanafunzi wamo darasani
  • Chakula ki mezani
  • Juma ana nyumba nzuri
  • Ndoo i kisimani
  • Hiki ndicho kitabu chake...

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kishazi huru kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.