Zuonosia
Zuonosia (kutoka Kiingereza: zoonosis, zoonotic desease) ni ugonjwa wa kuambukiza wenye asili ya mnyama unaosababisha ugonjwa wa binadamu.
Magonjwa ya zuonosia huenea kwa njia ya bakteria, virusi, fungi au vimelea[1].
Magonjwa hayo hutokea mara nyingi. Imekadidiriwa kuwa mnamo asilimia 60 za magonjwa ya kuambukiza yote ni ya zuonosia, yaani maambukizo hupitia wanyama au wadudu.[2]
Njia za maambukizi
[hariri | hariri chanzo]Maambukizi hutokea kiasili hasa kwa njia mbili
- mnyama mgonjwa anapitisha kiambukizi moja kwa moja hadi binadamu (mfano: kichaa cha mbwa kinapitishwa pale ambako virusi vyake vinaingia mwilini mwa binadamu, kwa kawaida mtu aking'atwa na mbwa mgonjwa).
- kupitia vekta (vector):
- kiambukizi kutoka mnyama mgonjwa kinahamia mnyama mwingine asiyegonjeka lakini anapitisha kiambukizi kwa binadamu (mfano: bakteria za tauni huambukiza panya; kutoka kwa panya mgonjwa huingia pia katika viroboto wanavyonyonya damu yao. Viroboto hao hawana tatizo na bakteria lakini wananyonya pia damu ya binadamu. Kwenye hatua hiyo kiambukizi kinapitishwa kwa binadamu na kusababisha tauni kwake.
- viambukizi vingine huishi ndani ya mnyama bila kusababisha ugonjwa kwake. Vimelea aina ya plasmodium vinavyosababisha malaria huishi ndani ya mbu za jenasi anopheles. Wakati wa kumdunga mtu mbu anapitisha kwa binadamu vimelea hivyo ambavyo vinasababisha homa ya malaria.
Magonjwa mbalimbali ya zuonosia
[hariri | hariri chanzo]Magonjwa yanayosababishwa na chakula
[hariri | hariri chanzo]Magonjwa mengi yanayotokana na chakula ni magonjwa ya zuonosia. Hapo mwanadamu anagonjeka kutokana na kula kitu ambacho kilitoka kwa mnyama mgonjwa.
Viambukizi vya kawaida ambavyo husababisha magonjwa kupitia chakula ni bakteria wa salmonella, campylobacter, na escherichia coli (E. coli). Mayai, samaki, nyama ya kuku, na maziwa vinaweza kubeba bakteria hao na kusababisha magonjwa yanayotokana na chakula, kama usumisho wa chakula, kwa wanadamu. [3] [4]
Magonjwa ya zuonosia yanayoambukizwa kupitia chakula ni pamoja na:
Ugonjwa | Pathojeni (kiambukizi) |
---|---|
Bruselosisi | bakteria ya brucella |
Kipindupindu | bakteria ya kipindupindu |
ugonjwa wa Creutzfeldt-Jakob | prioni |
listeriosisi | bakteria ya Listeria |
toksoplasmosisi | vimelea vya toxoplasma gondii |
Mara nyingi, watu wanaweza kuzuia maabukizi kupitia chakula kwa kukipika kwa muda wa kutosha na hivyo kuua bakteria au vimelea vilivyomo. [5]
Maambukizi ya moja kwa moja
[hariri | hariri chanzo]Yafuatayo ni mifano ya magonjwa ya zuonosia ambayo wanadamu wanaweza kuambukizwa moja kwa moja kutoka kwa wanyama wagonjwa walio hai.
Ugonjwa | Pathojeni (kiambukizi) |
---|---|
kimeta (anthrax) | bakteria ya bacillus anthracis |
homa ya mafua (influenza) | virusi vya influenza A |
homa ya Lassa | virusi vya lassa |
kichaa cha mbwa | virusi vya rabies |
toksoplasmosisi | vimelea vya toxoplasma gondii |
kifua kikuu | bakteria ya mycobacterium bovis |
Magonjwa ya zuonosia yanayoambuiza kupitia vekta
[hariri | hariri chanzo]Ugonjwa | Pathojeni | Kimelewa (mwenyeji) | Vekta | |
---|---|---|---|---|
ugonjwa wa malale | vimelea vya trypanosoma brucei rhodesiense | Wanyama mwitu na wa kufugwa mbaimbali | mbung'o | |
tauni (bubonic plague) | bakteria ya yersinia pestis | panya, rodentia | viroboto[6] | |
homa ya dengi | virusi vya dengue (flavi) | binadamu na nyani | mbu wa aedes [7] | |
borrelosia (borreliosis, Lyme desease) | bakteria ya borrellia | mamalia na ndege | papasi[8] | |
malaria | vimelea vya plasmodium | binadamu | mbu, hasa anopheles[9] | |
homa ya Naili magharibi (West Nile fever) | virusi vya Naili magharibi (West Nile virus) | hasa ndege | mbu[10] |
Magonjwa mapya kutokana na virusi badilifu
[hariri | hariri chanzo]Kuna virusi mbalimbali ambavyo kwa kawaida vinapatikana kwa wanyama vinavyoweza kubadili tabia kadhaa na kupata uwezo wa kuathiri binadamu.
Mabadiliko ya aina hiyo yametazamwa hasa kwa virusi vya influenza[11] vya ndege, nguruwe na farasi, halafu kwa virusi vya corona[12].
Wakati virusi vya wanyama vinapata uwezo wa kusambaa kutoka mtu hadi mtu, vinaweza kuathiri watu wengi kwa sababu ni "virusi vipya". Maana mwili hupambana na virusi kwa uwezo wa mfumo wa kingamaradhi (immune system) unaochungulia virusi na kutoa zindikomwili (antibodi) zenye uwezo wa kuzuia virusi. Mfumo wa kingamaradhi hukumbuka mashambulio ya miaka ya nyuma, lakini virusi vipya ni changamoto kwa mfumo huo. Kama virusi vipya kutoka mnyama fulani ni tofauti sana na vyote vilivyotangulia uwezo wake wa kusababisha hatari kali ya afya ni mkubwa. Hapa kuna uwezekano wa mlipuko wa maambukizi (epidemia, hata pandemia) jinsi ilivyotokea kwenye tauni ya karne za kati, na influenza ya 1918.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Toxoplasmosis". One Health. United States Centers for Disease Control and Prevention. Oktoba 18, 2013. Iliwekwa mnamo Februari 11, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Taylor L.H; Latham S.M. & Woolhouse M.E.J. 2001. Risk factors for human disease emergence. Philosophical Transactions of the Royal Society B: Biological Sciences 356 (1411): 983–989. [1]
- ↑ Humphrey T; O'Brien S; et al. 2007. "Campylobacters as zoonotic pathogens: A food production perspective". International Journal of Food Microbiology. 117 (3): 237–257. doi:10.1016/j.ijfoodmicro.2007.01.006. PMID 17368847.
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ Cloeckaert A 2006. "Introduction: emerging antimicrobial resistance mechanisms in the zoonotic foodborne pathogens Salmonella and Campylobacter". Microbes and Infection. 8 (7): 1889–1890. doi:10.1016/j.micinf.2005.12.024. PMID 16714136.
{{cite journal}}
: CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ "Toxoplasmosis". One Health. United States Centers for Disease Control and Prevention. Oktoba 18, 2013. Iliwekwa mnamo Februari 11, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Plague". WHO.int. World Health Organization. Novemba 2014. Iliwekwa mnamo Februari 11, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Vector-borne viral infections". World Health Organization. 2016. Iliwekwa mnamo Februari 11, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Tilly K; Rosa PA. et al. 2008 (Juni 2008). "Biology of infection with Borrelia burgdorferi". Infectious Disease Clinics of North America. 22 (2): 217–34, v. doi:10.1016/j.idc.2007.12.013. PMC 2440571. PMID 18452798.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ "Malaria". WHO.int. World Health Organization. 2016. Iliwekwa mnamo Februari 11, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "West Nile virus". WHO.int. World Health Organization. Julai 2011. Iliwekwa mnamo Februari 11, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Zoonotic influenza, tovuti ya WHO, iliangaliwa Februari 2020
- ↑ Coronavirus, tovuti ya WHO, iliangaliwa Februari 2020
Tovuti za Nje
[hariri | hariri chanzo]- ORIGINS OF MAJOR HUMAN INFECTIOUS DISEASES, tovuti ya National Center for Biotechnology Information, U.S. National Library of Medicine
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zuonosia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |