[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Paa (Bovidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 09:27, 2 Julai 2010 na Xqbot (majadiliano | michango) (roboti Nyongeza: rw:Impara; cosmetic changes)
Kigezo:Taxobox/species
Impala
Scientific classification
Kingdom: Animalia
Phylum: Chordata
Class: Mammalia
Order: Artiodactyla
Family: Bovidae
Subfamily: Aepycerotinae
Gray, 1872
Genus: Aepyceros
Sundevall, 1847
Species: A. melampus
Binomial name
Aepyceros melampus
(Lichtenstein, 1812)
Subspecies
Range map

Paa (Aepyceros melampus Kigiriki αιπος, aipos "juu" κερος, ceros "pembe" + melas "nyeusi" pous "mguu") ni swara ambaye si mkubwa sana kutoka Afrika. Jina Implala ambalo ni jina la Paa kwa Kiingereza linatoka kutoka lugha ya Kizulu na linamaanisha "Swara". Wao hupatikana katika savanna misitu nene nchini Kenya, Tanzania, Swaziland, Msumbiji, Namibia ya kaskazini, Botswana, Zambia, Zimbabwe, kusini mwa Angola, kaskazini mashariki mwa Afrika Kusini na Uganda. Paa wa kawaida wanaweza kupatikana katika idadi ya hadi 1,600,000 barani Afrika [1]


Taksonomia

Hapo awali, wanataksonomia waliwaweka Paa katika jamii sawa na swara, kob na hartebeest. Hata hivyo ilikuja kugunduliwa kwamba paa ni tofauti sana kutoka jamii hizi zote za swara ndiposa paa ikawekwa katika jamii yake yenyewe, Aepycerotini ,mtawalia. Jamii hii kwa sasa imepandishwa cheo kuwa familia kamili.


Kwa kawaida Spishi za aina mbili hutofautishwa, ambazo huegemewa na uchambuzi wa mitochondrial DNA.

  • Paa aliye na sura nyeusi( Black-faced Impala Aepyceros melampus petersi )
  • Paa wa kawaida ((Common Impala) Aepyceros melampus melampus )


Mwonekano

Paa dume kutoka Kruger National Park, Afrika ya Kusini.

Paa wanaurefu wa kati ya sentimita 73 na 92. Wastani wa uzito wa paa wa kiume ni takriban kilo 46 hadi 76 huku paa wa kike wakiwa na uzito wa takriban kilo 37 hadi 50. Rangi yao kwa kawaida ni nyekundu na kahawia(ndiposa wakapewa jina la Kiafrikana la "Rooibok" ), wana ubavu mwepesi na tumbo nyeupe alama "M" katika ngozi zao . Paa wa kiume, ambao wanajina sawa kama wa kondoo waume, wanapembe unao fanana kama aina fulani ya chombo cha muziki kinachojulikana kama 'lyre' kwa lugha ya kimombo ambayo inaweza kufikia urefi wa sentimita 90 . Paa wa kike, ambao wanajina sawa na kondoo wa kike, hawana pembe.


Paa weusi

Paa weusi, hupatikana katika maeneo machache sana barani Afrika, na aina ya paa hawa ni nadra sana na wana mwili ambao ni mweusi tititit. Hifadhi ya wanyama ya kibinasi ya Botlierskop Binafsi nchini Afrika Kusini ina zaidi ya paa weusi 150 na hata zaidi ya Paa wekundu. Wanyama hawa wanaweza kufomu makundi makubwa ya zaidi ya paa 100, lakini kwa kawaida idadi ya mkusanyijo wao huwa 20. Kidude cha ukoo kinachopatikana katika Paa huwapa rangi yao.


Mazingira

Paa ni miongoni mwa spishi amboa wametamalaki katika aina nyingi za savanna. Wanaweza kukabiliana na mazingira tofauti kwa kuwa kwa kuwa walaji wa nyasi katika baadhi ya maeneo. Wao hula majani na nyasi wakati rangi ya majani na nyasi ni kijani na ambao unakuwa .


Vikundi vya paa hutumia maeneo maalum kwa matumizi yao. Paa huwa hodari wakati wote wa usiku na mchana na wanategemea maji. Mifugo ni huashiria kwa kawaida kuwa kuna maji karibu. Paa wanaweza kustawi katika maeneo ambayo walaji nyasi pekee hawezi kuishi.

Paa mke kutoka kwa Kruger National Park, Afrika ya Kusini.


hurukaruka huku na huko ili kuwavurugia wanyama ambao wanaweza kuwala. Wao wanaweza kuruka kwa umbali wa zaidi ya mita 10 mita (fiti 33) na urefu wa mita 3(fiti 9). Chui, Duma, simba na mbwa mwitu ndio wanyama ambao huwawinda Paa. Paa wanaweza kufikia kasi ambao wastani wake ni maili 50 hadi 55 kwa saa moja (kilomita 80 hadi 90 kwa saa mija) [2] ili kuwaepuka wanyama ambo wanaweza kuwala.


Muundo wa kijamii na uzazi

Paa wa kike na paa wale wachanga kufomu vikundi vya paa mia moja au mia mbili. Wakati wa chakula upo kwa wingi, paa wa kiume wazima wataimarisha wilaya na kuwazunguka paa wa kike na kuwafukuza paa kike ambao si wa jamii kundi hilo pamoja na wanyama wengine ambao wanaweza kuwala. Pia wao huwafukuza paa wa kiume wengine ambo wamebaleha. Paa wa kiume hujaribu kuzuia paa wa kike yeyote anayejaribu kuondoka katika wilaya ambao walikuwa wameutenga. Katika misimu wa ukavu, wilaya hizi hutelekezwa na kuachwa kwani vikundi hivi vya paa husafiri mbali ili kutafuta chakula. Vikunde vikubwa vya paa huanzishwa na hujumuisha paa wa kike na wa kiume.


Paa vijana wa kiume ambao wamefanywa kuacha vikundi vyao vya awali hufomu kundi yao ya karibu takriban paa thelathini binafsi. Paa wa kiume ambao wanaweza kutawala na kutamalaki vikundi vyao huwa wagombeaji kwa ajili ya kuchukua udhibiti wa wilaya zao.

Faili:GrantsGazelle1.jpg
Paa kuchungia katika Maasai Mara, Kenya
Paa kurukaruka huku nchini Kenya

Msimu wa kuzaana wa Paa, ambao pia hujulikana kama rutting kwa lugha ya Kiingereza, huanza wakati unaelekea mwisho wa msimu wa mvua mwezi wa Mei. Mambo haya yote kwa kawaida hudumu kwa muda wa takriban wiki tatu. Huku paa wachanga wakizaliwa baada ya miezi saba, mama yao ana uwezo wa kuchelewa kujifungua kwa nyongeza ya mwezi moja kama hali ni mbaya. Wakati wa kujifungua paa wa kike hujitenga mwenyewe kutoka katika kundi ya paa wengine licha ya jitihada mbalimbali ya paa wa kiume kumzuia kuondoka katika wilaya yao. Paa wa kike ambaye amekuwa mama kumweka mwanawe aliyezaliwa katika doa kwa siku chache au hata kumwacha mwanawe mafichoni kwa siku, wiki kadhaa au zaidi kabla ya kurudi kwa kundi la paa wenzake. Wanawe wachangwa watajiunga na kikundi cha paa wengine na watakwenda kwa mamao tu wakati kuna shida au wakati wananjaa na wanahitaji kula. Paa wachanga hunyonya matiti ya mamao kwa muda wa kati ya miezi 4 hadi 6. Paa wa kike ambao hukomaa wanalazimika kujiondoa katika kikundi hicho na kujiunga na kundi mpya ya paa ya wanaume pekee.


Hifadhi ya picha


Tazama Pia

  • Paa mweusi


Marejeo


Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.