Ndege (mnyama)
Ndege (Aves) | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ndege (Buabua-kishungi mkubwa)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusungeli na oda za juu: |
Ndege ni wanyama wenye uti wa mgongo (chordata) na miguu miwili wanaozaliana kwa kutaga mayai.
Biolojia inawapanga katika ngeli ya Aves.
Ndege wameenea kote duniani kuanzia Aktiki hadi Antaktiki.
Ndege mdogo huwa na sentimita 5 tu na ndege mkubwa ana urefu wa mita mbili na nusu.
Ndege huwa na manyoya, mdomo bila meno, mayai yenye ganda gumu, moyo wenye vyumba vinne na mifupa myepesi ambayo ni imara.
Ndege walio wengi wana uwezo wa kuruka hewani na maumbile yao yanalingana na kusafiri hewani. Ila tu aina chache zimepoteza uwezo wa kuruka kwa mfano mbuni, ngwini na ndege kadhaa wa visiwani.
Aina nyingi za ndege huwa na misafara ya kila mwaka, kwa mfano korongo mweupe husafiri kila mwaka kati ya Afrika na Ulaya.
Uainishaji
hariri- Ngeli Aves: Ndege
- Nusungeli Neornithes: Ndege waliopo hadi sasa
- Oda ya juu Palaeognathae:
- Oda Struthioniformes: K.m. mbuni, emu, kiwi, n.k.
- Oda Tinamiformes: Tinamu
- Oda ya juu Neognathae:
- Oda Anseriformes: Mabata
- Oda Galliformes: K.m. kanga, kwale, tausi, kuku, n.k.
- Oda Charadriiformes: K.m. vitwitwi, chekehukwa, shakwe, sululu, n.k.
- Oda Gaviiformes: Wazamaji
- Oda Podicipediformes: Vibisi
- Oda Procellariiformes: Albatrosi, walinzi, walinzi wazamaji na ninga-bahari
- Oda Sphenisciformes: Ngwini
- Oda Pelecaniformes: Wari, kwarara, domomwiko, vumatiti, yangeyange, vingoyo na koikoi
- Oda Phaethontiformes: Ndege-mawingu
- Oda Suliformes: Ndegejinga, minandi, minandi-pwani na mbizi
- Oda Ciconiiformes: Makorongo
- Oda Cathartiformes: Tumbusi wa Dunia Mpya
- Oda Phoenicopteriformes: Heroe
- Oda Accipitriformes: K.m. tai, tumbusi, vipanga, shakivale n.k.
- Oda Falconiformes: Kozi
- Oda Gruiformes: Makorongo, viluwiri, kukuziwa, shaunge, fuluwili na viguudau
- Oda Otidiformes: Tandawala
- Oda Mesitornithiformes: Mesite
- Oda Pterocliformes: Firigogo
- Oda Columbiformes: Njiwa, ninga, hua na pugi
- Oda Psittaciformes: Kasuku, kwao na cherero
- Oda Cuculiformes: Kekeo, dudumizi na kua
- Oda Musophagiformes: Shorobo na gowee
- Oda Opisthocomiformes: Hoatzini
- Oda Strigiformes: Bundi, kungwi, vitaumande na mititi
- Oda Caprimulgiformes: K.m. virukanjia, potuu, ndege-mafuta, domo-chura n.k.
- Oda Apodiformes: Teleka na kolibri
- Oda Coraciiformes: Viogajivu, jore, keremkerem, detepwani, kurea na midiria
- Oda Bucerotiformes: Hondohondo, kwembekwembe, fimbi, mumbi, goregore, domomundu na hudihudi
- Oda Piciformes: Vigong'ota, viseleagofu, viongozi na walembe
- Oda Trogoniformes: Lukungu
- Oda Coliiformes: Kuzumburu
- Oda Passeriformes: Zaidi ya nusu ya spishi za ndege, k.m. shomoro, kunguru, mikesha, chiriku n.k.
- Oda ya juu Palaeognathae:
- Nusungeli Neornithes: Ndege waliopo hadi sasa
Picha
hariri-
Ndege juu ya tawi katika Hifadhi ya Nyerere
-
Ndege wakipata chakula katika Hifadhi ya Nyerere
-
Ndege mwenye rangi juu ya tawi
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ndege (mnyama) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |