[go: up one dir, main page]

Mlembe
Mlembe mgongo-kahawia
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Piciformes (Ndege kama vigong'ota)
Familia: Indicatoridae (Ndege walio na mnasaba na viongozi)
Jenasi: Prodotiscus
J. Verreaux & E. Verreaux, 1855

Walembe ni ndege wadogo wa jenasi Prodotiscus katika familia Indicatoridae. Spishi zote zinatokea Afrika chini ya Sahara. Ndege hawa wana rangi za kijivu, kahawa na nyeupe. Wapo baina ndege wachache ambao hula nta ya wadudu-gamba. Hula wadudu na buibui pia, hata matunda mara kwa mara. Mwenendo wa kuongoza watu na wanyama kama nyegere mpaka masega ya nyuki haukuona kwa walembe.

Walembe hawatengenezi tago lao lenyewe. Jike huyataga mayai 1-3 katika kila moja la matago ya mviringo ya spishi nyingine za ndege, k.m. vinengenenge, videnenda, magamaga, vibwirosagi na chozi. Domo la kinda la mlembe lina kikulabu kinachotumika kwa kuyatoboa mayai ya mwenyeji na kuwaua makinda yake.

Spishi

hariri