Kua
Ndege wakubwa kiasi wa jenasi Coua, familia Cuculidae
Kua | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 11:
|
Kua (kutoka Kimalagasy: koa) ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Coua katika nusufamilia Phaenicophaeinae ya familia Cuculidae. Pengine wanaainishwa katika nusufamilia yao Couinae pamoja na kekeo-ardhi wa Asia (Carpococcyx). Jenasi pekee ya Bara la Afrika inayoainishwa katika Phaenicophaeinae ni Ceuthmochares (ukiki). Kua ni ndege wa Madagaska wanaofanana na kekeo. Wana mkia mrefu na miguu mirefu. Kidole cha tatu cha miguu yao kinaweza kukabili mbele au nyuma. Rangi kuu ni kijivu na/au buluu na wana ngozi tupu kuzunguka macho yenye rangi buluu. Kua hula mbegu, matunda madogo, wadudu na wanyama wadogo kama mijusi na vigeugeu. Kinyume na kekeo, kua hulijenga tago lao lenyewe. Jike huyataga mayai meupe 1-3 (2 mara nyingi zaidi).
Spishi za Afrika
hariri- Coua caerulea, Kua Buluu (Blue Coua)
- Coua coquereli, Kua wa Coquerel (Coquerel's Coua)
- Coua cristata, Kua Kishungi (Crested Coua)
- Coua c. maxima – inajulikana kutoka ndege mmoja tu, pengine imekwisha mwisho wa karne ya 20 au ndege hawa alikuwa chotara
- Coua cursor, Kua Mkimbiaji (Running Coua)
- Coua delalandei, Kua wa Delalande (Delalande's Coua) imekwisha sasa (mwisho wa karne ya 19)
- Coua gigas, Kua Mkubwa (Giant Coua)
- Coua olivaceiceps, Kua Utosi-zeituni (Olive-capped Coua)
- Coua reynaudii, Kua Paji-jekundu (Red-fronted Coua)
- Coua ruficeps, Kua Utosi-mwekundu (Red-capped Coua)
- Coua serriana, Kua Kidari-chekundu (Red-breasted Coua)
- Coua verreauxi, Kua wa Verreaux (Verreaux's Coua)
Spishi za kabla ya historia
hariri- Coua berthae, Kua wa Bertha (Bertha's Coua) – Mwisho wa Quaternary
- Coua primaeva, Kua wa Kale (Ancient Coua) – Mwisho wa Quaternary
Picha
hariri-
Kua buluu
-
Kua wa Coquerel
-
Kua kishungi
-
Kua mkimbiaji
-
Kua wa Delalande
-
Kua utosi-zeituni