Albatrosi
Albatrosi | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 4:
|
Albatrosi (kutoka Kiing.: albatross) ni ndege wakubwa wa bahari katika familia Diomedeidae. Baina ya spishi hizi yuko ndege wenye mabawa marefu kabisa kuliko ndege wote duniani. Albatrosi Mlizi ana mabawa ambayo mawili pamoja yana urefu wa sm 310 kwa wastani na urefu mkubwa kabisa uliopimwa ulikuwa sm 370. Rangi zao zinatofautiana kutoka nyeupe na mabawa kijivu hafifu hadi mwili wote kijivucheusi. Wana domo kubwa sana lenye ncha kwa umbo la kulabu. Mirija miwili ya pua inapitia pande zote mbili za domo.
Ndege hawa huenda mbali sana wakiruka angani na wanaweza kuzunguka dunia. Hawapigi mabawa sana baada ya kuruka, lakini wananyiririka kwa mabawa yaliyonyooshwa. Huwakamata ngisi, samaki na gegereka na hula mizoga pia. Kwa kawaida albatrosi huyatengeneza matago yao kwenye visiwa vya mbali visipokaa watu wala mamalia wengine. Kabla ya kujamiiana dume na jike hutenga dansi ya kanuni kaida. Jike hulitaga yai moja tu.
Spishi za Afrika
hariri- Diomedea amsterdamensis, Albatrosi wa Kisiwa Amsterdam (Amsterdam Albatross)
- Diomedea dabbenena, Albatrosi wa Tristan (Tristan Albatross)
- Diomedea epomophora, Albatrosi Mfalme (Southern Royal Albatross)
- Diomedea exulans, Albatrosi Mlizi (Wandering Albatross)
- Phoebetria fusca, Albatrosi Kijivucheusi (Sooty Albatros)
- Phoebetria palpebrata, Albatrosi Mgongo-kijivu (Light-mantled Albatros)
- Thalassarche bulleri, Albatrosi wa Buller (Buller's Albatross)
- Thalassarche carteri, Albatrosi Domo-njano wa Bahari ya Hindi (Indian Yellow-nosed Albatross)
- Thalassarche cauta, Albatrosi Utosi-mweupe (Shy Albatross)
- Thalassarche chlororhynchos, Albatrosi Domo-njano wa Bahari ya Atlantiki (Atlantic Yellow-nosed Albatross)
- Thalassarche chrysostoma, Albatrosi Kichwa-kijivu (Grey-headed Albatross)
- Thalassarche melanophris, Albatrosi Nyusi-nyeusi (Black-browed Albatross)
- Thalassarche salvini, Albatrosi wa Salvin (Salvin's Albatross)
Spishi za mabara mengine
hariri- Diomedea antipodensis (Antipodean Albatross)
- Diomedea sanfordi (Northern Royal Albatross)
- Phoebastria albatrus (Short-tailed Albatross)
- Phoebastria immutabilis (Laysan Albatross)
- Phoebastria irrorata (Waved Albatross)
- Phoebastria nigripes (Black-footed Albatross)
- Thalassarche eremita (Chatham Albatross)
- Thalassarche impavida (Campbell Albatross)
Picha
hariri-
Albatrosi wa Kisiwa cha Amsterdam
-
Albatrosi wa Tristan
-
Albatrosi mfalme
-
Albatrosi mlizi
-
Albatrosi kijivucheusi
-
Albatrosi mgongo-kijivu
-
Albatrosi wa Buller
-
Albatrosi domo-njano wa Bahari ya Hindi
-
Albatrosi utosi-mweupe
-
Albatrosi domo-njano wa Bahari ya Atlantiki
-
Albatrosi kichwa-kijivu
-
Albatrosi nyusi-nyeusi
-
Albatrosi wa Salvin
-
Antipodean (Gibson's) albatros
-
Northern royal albatros
-
Short-tailed albatross
-
Laysan albatross
-
Waved albatross
-
Black-footed albatross
-
Chatham albatross
-
Campbell albatross