Mvua asidia
Mvua asidia ni hali ya mvua ambako kemikali katika angahewa zinaungana na unyevu ndani ya hewa na kusababisha maji ya mvua kuwa na kiasi kikubwa cha asidi.
Mvua asidia huathiri vibaya mimea, wanyama wa mitoni au maziwani na pia majengo au barabara. Inasababishwa hasa na hewa chafu kutoka viwanda, mashine na mitambo inayotoa sulfuri na nitrojeni na kuziingiza hewani.
Mvua ya kawaida kuwa mvua asidia
[hariri | hariri chanzo]Kwa kawaida mvua ina asidi kidogo ndani yake kwa sababu hewani kuna gesi ya dioksidi kabonia (CO2) inayomenyuka na maji kuwa asidi kabonia. Hii ni asidi hafifu. Kiwango cha asidi hupimwa kwa thamani pH na mvua ya kawaida huwa na thamani pH ya 5.2 hadi 5.6.
H2O (l) + CO2 (g) → H2CO3 (aq)
Oksidi za sulfuri na nitrojeni kutokana na hewa chafu zinasababisha kutokea kwa asidi kali zaidi kama asidi salfuria (H2SO4) na asidi ya naitrojeni ndani ya maji ya mvua.
Oksidi za sulfuri zinatokana hasa kutokana na kuchomwa kwa makaa mawe na mafuta ya petroli kwa umbo la petroli na diseli.
- 2 SO2 + O2 → 2 SO3
- SO3 + H2O → H2SO4
Katika kila tendo la kuchoma kitu kuna mmenyuko wa nitrojeni ya hewani na oksijeni:
- 2 NO2 + H2O → HNO2 + HNO3
- N2O4 + H2O → HNO2 + HNO3
Asidi salfuria husababisha theluthi mbili na asidi ya nitrojeni theuthi moja ya asidi katika mvua asidia.
Athari za mvua asidia
[hariri | hariri chanzo]Mimea
[hariri | hariri chanzo]Mvua asidia huongeza kiwngo cha asidi katika ardhi. Asidi hii inatoa ioni za metali nzito kutoka kampaundi asilia ya udongo ambazo ni sumu kwa mimea kama zinatokea nje ya kampaundi. Mizi midogo ya mimea inaharibika na kwa njia hii uwezo wa mmea kujilisha unapungua. Nguvu yake inapungua na mmea hushambuliwa kirahisi na magonjwa. Uwezo wa kupambana na wadudu au ugumu wa hali ya hewa kama ukame, joto au baridi inayozidi kiwango cha kawaida.
Msituni matokeo ya mvua asidia yameonekana kwa kukauka kwa majani kwenye matawi.
Magimba ya maji
[hariri | hariri chanzo]Mito na maziwa huongezeka asidi kutokana na mvua asidia. Kationi metalia huzidi majini na kuwa kama sumu kwa viumbe wanaoishi mle.
Spishi kadhaa zinaathirikia zaidi na kupungukiwa. Kama thamani pH inapungua chini ya 5 samaki nyingi hazizai tena; mayai ya samaki hayawezi kukomaa hakuan samaki wadogo tena.
Maziwa kadhaa katika Skandinavia yalionekana tayari kuwa bila samaki au wanyama wengine kwa sababu hewa chafu kutoka Ulaya ya Kati ilifika hapa na kusababisha kiasi kikuba cha mvua asidia.
Kuna hofu ya kwamba mito inaweza kuingiza polepole maji asidia kwenye bahari hadi hata bahari kuzidi asidi. Hapa hatari kubwa ni ya kwamba maganda ya viumbe kama vidondo, vyondo na konokono ambayo ni ya chokaa yatayeyushwa na spishi hizi kupotea. Hii ingeharibu mtungo wa chakula baharini.
Majengo
[hariri | hariri chanzo]Kiwango cha asidi katika mvua ni hatari kwa mawe mengi yanayotumiwa katika ujenzi laini pia kwa saruji.
Mawe ya ujenzi mara yingi ni aina za gange (mawe ya chokaa); mapambo mengi kwenye ujenzi ni ya marumaru; saruji ina koasi kikubwa cha chokaa ndani yake. Haya yanashambuliwa na asidi katika mvua asidia. Uso wa jengo linaanza kuharibika kwanza lakini maji asidia inaingia pia ndani ya kuta za saruji na kula chuma kilichomo ndani yake.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mvua asidia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |