[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Lucas Vázquez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vázquez baada ya kushinda Ligi ya Mabingwa ya UEFA na Real Madrid mnamo 2018

Lucas Vázquez Iglesias (aliyezaliwa 1 Julai 1991) ni mchezaji wa soka wa Hispania ambaye anachezea klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania kama winga wa kulia.

Vázquez aliwakilisha Hispania kwenye Euro 2016.

Real Madrid

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Curtis huko Galicia, Vázquez aliwasili katika mfumo wa vijana wa Real Madrid mwaka 2007, akiwa na umri wa miaka 16. Alikuwa na mafanikio katika msimu wa 2010-11 na timu C na kampeni iliyofuata, alifunga mabao 22 na kupandishwa daraja.

Espanyol

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Agosti 19, 2014, Vázquez alikopwa kwa RCD Espanyol ya La Liga, kwa kipindi cha muda mrefu. Alicheza kwanza katika mashindano ya Agosti 30 2014, akiwa kama mfungaji wa pili dhidi ya Sevilla FC katika ushindi wa nyumbani.

Vázquez alifunga bao lake la kwanza waliposhinda 2-0 nyumbani dhidi ya Real Sociedad.

Kurudi Real Madrid

[hariri | hariri chanzo]
Lucas Vazquez akiwa Real Madrid

Mnamo tarehe 30 Juni 2015, Real Madrid ilisaini mkataba na Vazquez na kurudi RealMadrid. Alicheza mechi yake ya kwanza mnamo 12 Septemba 2015 na walishinda 6-0 dhidi ya timu yake ya zamani Espanyol.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lucas Vázquez kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.