[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Dimitri Mendeleyev

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dmitri Mendeleev

Dimitri Ivanovich Mendeleyev (kwa Kirusi Дми́трий Ива́нович Менделе́ев; Tobolsk, 8 Februari {kwa K.J. 27 Januari) 1834Sankt Petersburg, 2 Februari (K.J. 20 Januari) 1907) alikuwa mtaalamu wa kemia kutoka nchini Urusi.

Mendeleev alikuwa mtu wa kwanza wa kupanga elementi za kikemia katika jedwali la elementi. Baada ya kumaliza jedwali aliweza kutabiri kuwepo kwa elementi tatu zilizokuja kugunduliwa baadaye.

Alifuata masomo ya theolojia na ualimu akawa mwalimu wa sayansi shuleni. Aliendelea kusoma kemia huko Paris na Heidelberg akichungulia hasa tabia za gesi.

Baada ya kurudi Urusi alipata nafasi ya kufundisha kwenye chuo cha teknolojia Sankt Peterburg na pia kwenye chuo kikuu alipoendelea kuwa profesa. Alipata sifa nyingi kimataifa lakini hakuendelea kupewa nafasi katika akademia ya sayansi kwa sababu ya talaka katika ndoa yake.

Mwaka 1890 alijiuzulu kwenye chuo kikuu kwa sababu alipinga kuingilia kwa serikali katika mambo ya chuo kikuu.

Mwaka 1893 aliombwa kusimamia taasisi ya kusanifisha vipimo ya Urusi. Alianzisha mfumo wa vipimo vya mita nchini akatunga pia kanuni jinsi ya kutengeneza vodka.

Aliaga dunia mwaka 1907. Elementi 101 iliitwa kwa heshima yake "Mendelevi" na pia kasoko ya Mendeleyev kwenye mwezi ilipewa jina kwa kumbukumbu yake.

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dimitri Mendeleyev kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.