Vitus Bering
Vitus Jonassen Bering (aliitwa pia jina la Kirusi: Ivan Ivanovich Bering; 1681 - 1741[1]) [2] alikuwa baharia na mpelelezi kutoka nchini Denmark aliyejiunga na jeshi la majini la Urusi mnamo mwaka 1704. Wakati wa Vita Vikuu vya Kaskazini alijipatia sifa na kupandishwa cheo kuwa kamanda.
Msafara wa kwanza wa Kamchatka
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka wa 1639 wawindaji Warusi walivuka Bahari Pasifiki kutoka Siberia hadi Amerika ya Kaskazini . [3] Tsar Peter I wa Urusi aliposikia kuhusu safari hiyo alitaka kuwa na uhakika kuhusu ukweli wake. Mnamo 1724 alituma msafara wa kwanza kwenda Kamchatka (1725-30) ulioongozwa na Bering. Shabaha moja ilikuwa kuona kama Siberia imeunganika na Amerika Kaskazini. Walisafiri kwanza hadi Rasi ya Kamchatka ambapo walijenga meli kwa ajili ya upelelezi. Mnamo 1728 Bering alisafiri kaskazini kwa kutosha ili kugundua kuwa Siberia na Amerika Kaskazini (Alaska) haziunganiki. [1] Hapo aliona sehemu ya bahari inayotenganisha Asia na Amerika iliyopokea baadaye jina la Mlangobahari wa Bering kwa heshima yake.
Msafara wa pili wa Kamchatka
[hariri | hariri chanzo]Msafara wa pili wa Kamchatka (1733-43) ilikuwa safari kubwa sana ya kisayansi. Iliongozwa pia na Bering. Msafara huo, ulipokuwa njiani, ulituma makundi madogo ya wapelelezi kwenda pande mbalimbali waliochora kwa mara ya kwanza ramani za pwani za Siberia na Bahari Pasifiki. Bering alituma pia meli hadi Japani na Amerika.[1] Bering mwenyewe alifikia Alaska mnamo 1741. Katika safari ya kurudi ilibidi wasimame kwenye kisiwa kilichopokea baadaye jina la Kisiwa cha Bering. Walipokaa kisiwani karibu nusu ya mabaharia wote walifariki, pamoja na Bering.
Mnamo 1991, wataalamu wa akiolojia kutoka Denmark walikuta kaburi lake.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 "Vitus Bering". Ministry of Foreign Affairs of Denmark. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-18. Iliwekwa mnamo 15 Desemba 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>
tag; name "MFAD" defined multiple times with different content - ↑ Peter Lauridsen, Vitus Bering: The Discoverer of Bering Strait (Freeport, NY: Books for Libraries Press, 1969), p. 77
- ↑ Jennifer Speake, Literature of Travel and Exploration, Vol 2 (New York; London: Fitzroy-Dearborn Publishers, 2003), p. 897
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vitus Bering kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |