Ufuta
Mandhari
Ufuta (pia huitwa benne) ni mmea unaochanua maua. Ufuta hujitokeza sana katika mapori hasa katika nchi za Afrika na idadi ndogo zaidi nchini India.
Mara nyingi ufuta huota sana katika maeneo ya kitropiki duniani kote na unalimwa kwa ajili ya mbegu zake zinazoliwa, ambazo hukua kwenye maganda. Uzalishaji wa dunia mwaka wa 2018 ulikuwa tani milioni 6 za metriki (tani ndefu 5,900,000; tani fupi 6,600,000), huku Sudan, Myanmar, na India zikiwa wazalishaji wakubwa zaidi.
Mbegu za ufuta ni mojawapo ya mazao ya zamani zaidi ya mbegu za mafuta yanayojulikana, yaliyopandwa tangu zaidi ya miaka 3,000 iliyopita. Sesamum ina spishi nyingine nyingi, nyingi zikiwa za porini na asili yake ni Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.[1]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The Plant List: A Working List of All Plant Species". Retrieved 14 January 2015. Merriam-Webster Benne