[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Wanyamwanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wanyamwanga ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Songwe, Wilaya ya Momba, na Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.

Lugha yao ni Kinyamwanga, jamii ya Kifipa.

Kabila hilo ni zao la makabila zaidi ya manne likiwemo kabila la Wawemba wanaopatikana kaskazini mwa Zambia, Wamambwe katika eneo la Chisitu, Kapele, Namchinka, Kasama na Mambwe.

Pia ni kabila la asili lililoanzisha mji wa Tunduma. Ukiwa unaelekea mkoani Rukwa kutokea Tunduma vijiji vya jamii ya Wanyamwanga ni Ndarambo, Msungo almaarufu kijiji cha wachawi, Mpui ya Unyamwanga, Rwasho ulipokatiza mto Momba ambao ndio uliobeba jina la wilaya mpya, Tunko, Mkutano ambapo ndipo mpaka wa mkoa wa Rukwa na wilaya ya Momba, kisha Laela, Mnadani na Mpui ya unyamwanga.

Upande wa kaskazini ni bonde la Msangano, delta ya mto Nkana, Kamsamba na vijiji vyake.

Jamii ya Wanyamwanga ni watu wakarimu sana, ambao ukifika kwao wajisikia uko nyumbani. Huheshimu familia na hali za kibinadamu. Ni kabila la ufugaji na kilimo kwa pamoja.

Chifu wa kabila hilo anaitwa mwene Siyame: cheo chake ni Chikanamlilo, na waziri mkuu ni Simwanza ambaye hutumika katika matambiko na kuita mvua.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanyamwanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.