Wandengereko
Wandengereko ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi kusini kwa Dar es Salaam katika Mkoa wa Pwani: Wilaya ya Rufiji, Wilaya ya Mkuranga, Wilaya ya Kibiti na Wilaya ya Mafia. Katika wilaya za Kibiti na Rufiji asilimia kubwa kabisa ni Wandengereko. Pia wako wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam maeneo ya Tandika mpaka Mbagala.
Lugha yao ni Kindengereko.
Wandengereko wapo karibu 700,000. Ni ndugu wa damu na Wamatumbi: tofauti yao ni kwamba kabila moja linaishi bondeni na lingine milimani; ndio Mmatumbi, maana ya Itumbi ni mlima ambao walikuwa wanaitwa na wenzao wa bondeni ambao ni Wandengereko.
Tena Wandengereko wapo wa bondeni ambao wanaitwa Warufiji maana wamepitiwa na mto Rufiji na Wamagongo yaani walio juu .
Koo za Kindengereko ni Momboka, Mkumba, Mzuzuri, Machela, Mkele, Mketo, Mpeta, Mpendu, Mbonde, Ipombo, Limbatike, Mponjo, Rwambo/Lwambo, Ngunde, Njechele, Songana, Ndembo, Nongwa, Kitingi, Matimbwa, Ungando, Kitambulio, Muki, Mminge, Mtulia, Mpogo, Kirungi n.k.
Watani wa Wandereko ni hasa makabila ya mikoa ya Tanzania kusini kama Wamakonde, Wayao, Wangindo, Wamakua, Wahehe, Wamwera, Wangoni, lakini pia Wasukuma wa Tanzania kaskazini magharibi.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wandengereko kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |