[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Raheem Sterling

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Raheem Sterling akiwa Liverpool.

Raheem Shaquille Sterling (alizaliwa mnamo 8 Desemba 1994) ni mchezaji wa soka wa Uingereza ambaye anachezea timu ya Chelsea F.C. na timu ya taifa ya Uingereza.

Alipokea tuzo ya Golden boy mwaka 2014 kutoka kwa waandishi wa habari wa pan huko London, wakimtambua kuwa mchezaji bora chini ya umri wa miaka 21 anayecheza Ulaya.

Alizaliwa huko Jamaica, Sterling alihamia London akiwa na umri wa miaka mitano na kuanza kazi yake huko Queens Park Rangers kabla ya kusainiwa na Liverpool F.C. mwaka 2010.

Mnamo Julai 2015, kufuatia mgogoro wa muda mrefu juu ya mkataba mpya, alisainiwa na Manchester City kwa uhamisho ambao unaweza kufikia £ milioni 49, ada ya uhamisho ya juu zaidi iliyolipwa kwa mchezaji wa Uiingereza. Mwaka 2020, Sterling anajiunga na Chelsea kwa £ milioni 47.5.[1]

Amezitumikia timu za taifa za Uingereza kuanzia chini ya umri wa miaka 16, miaka 21 hadi kucheza Kombe la Dunia la FIFA 2014, 2018 na 2022.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Raheem Sterling kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. https://www.skysports.com/football/news/11668/12647321/raheem-sterling-chelsea-sign-forward-from-man-city-for-gbp47-5m