[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Moskovi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Moskovi (Moscovium) ni elementi sintetiki yenye alama Mc na namba atomia 115. Hali halisi haiko duniani isipokuwa kwa muda mfupi ikitengenezwa katika maabara. Iliundwa kwa mara ya kwanza mnamo 2003 na kundi la wanasayansi wa Urusi na Marekani waliofanya kazi pamoja kwenye Taasisi ya pamoja ya utafiti wa nyuklia (JINR) huko Dubna, Urusi.

Watafiti walifyatua ioni za Kalisi Ca-48 dhdi ya Ameriki Am-243 wakaunda atomu nne za Moskovi. Atomi hizu zilibungua katika muda wa milisekunde 100 kwa kutoa vyembe vya alpha hadi kuwa Nihoni. [1] [2]

Mwaka 2016, elementi hiyo mpya ilipewa jina rasmi kwa heshima ya Moscow Oblast, mkoa ambako JINR iko. [3]

Moskovi ni elementi nururifu sana; isotopi yake iliyo thabiti zaidi huwa na nusumaisha ya sekunde 0.65 pekee.[4]

Hakuna tabia za kifizikia au kikemia zilizoweza kutazamwa; hii ni kwa sababu ya uzalishaji mdogo na gharama kubwa [5] na ukweli kwamba hubungua haraka sana.

  1. Oganessian, Yu. Ts.; Utyonkov, V. K.; Lobanov, Yu. V.; Abdullin, F. Sh.; Polyakov, A. N.; Shirokovsky, I. V.; Tsyganov, Yu.; Gulbekian, G.; Bogomolov, S. (2004). "Experiments on the synthesis of element 115 in the reaction 243Am(48Ca,xn)291−x115" (PDF). Physical Review C. 69 (2): 021601. Bibcode:2004PhRvC..69b1601O. doi:10.1103/PhysRevC.69.021601. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-03-07. Iliwekwa mnamo 2020-03-30. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |displayauthors= ignored (|display-authors= suggested) (help)
  2. Oganessian (2003). "Experiments on the synthesis of element 115 in the reaction 243Am(48Ca,xn)291−x115" (PDF). JINR Preprints. {{cite journal}}: Unknown parameter |displayauthors= ignored (|display-authors= suggested) (help)
  3. "IUPAC Is Naming The Four New Elements Nihonium, Moscovium, Tennessine, And Oganesson". IUPAC. 2016-06-08. Iliwekwa mnamo 2016-06-08.
  4. Oganessian, Y.T. (2015). "Super-heavy element research". Reports on Progress in Physics. 78 (3): 036301. Bibcode:2015RPPh...78c6301O. doi:10.1088/0034-4885/78/3/036301. PMID 25746203.
  5. Subramanian, S. "Making New Elements Doesn't Pay. Just Ask This Berkeley Scientist". Bloomberg Businessweek. Iliwekwa mnamo 2020-01-18.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Moskovi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.