[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Huduma ya ujumbe mfupi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Simu inapokea ujumbe mfupi wa maandishi.

Huduma ya ujumbe mfupi au huduma ya ujumbe mfupi wa maandishi (kutoka Kiing. SMS kwa short messaging service ) ni aina ya mawasiliano yanayotumika katika simu za mikononi. Yanafahamika sana kwa kuitwa "arafa" au "ujumbe mfupi". Ukiwa na SMS, mtu mmoja anaweza kumtumia mtu mwingine ujumbe wa maandishi.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Utafiti kuhusu huduma ya ujumbe mfupi kwa simu ilianzia miaka ya 1980. Ilivumbuliwa na shirika la Franco German GSM chini ya uongozi wa Friedhelm Hillebrand na Bernard Ghillebaert. Ujumbe mfupi wa kwanza ulitumwa naye mtafiti Neil Papworth mnamo 3 Desemba 1992 kwa mwenzake Richard Jarvis huku akimtakia Krismasi yenye fanaka. Maneno ya huduma hii fupi ilikuwa 'Merry Christmas'.

Matumizi ya ujumbe mfupi yanakwenda pole mno, kwa kuwa kwa kawaida watu wengi hupenda kutumia njia ya kupiga simu ya sauti badala ya kutuma ujumbe mfupi. Vilevile kuna mipaka ya utumaji maandishi yasiyozidi 160.[1] Ukituma ujumbe mrefu zaidi huhesabiwa kama jumbe zaidi ya moja, ambapo mtumiaji atatakiwa alipe zaidi ya ujumbe mmoja.

Jumbe fupi hutumwa kwa simu nyingine iwapo simu ya kawaida haikubali au inatumika sana. Ijapokuwa kuna baadhi ya watu wao huwa mahodari wa kutuma jumbe za kawaida. Matumizi ya jumbe fupi, huenda mtu yupo sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na hawezi kuongea mbele yao, basi atatumia huduma ya ujumbe mfupi kumfahamisha huyo mtumiaji mwenzake juu ya suala fulani nyeti kwa kutumia huduma hii. Gharama za jumbe itategemea na mtandao unaokupa huduma. Baadhi ya mitandao hutoa jumbe bila kikomo kwa kujiunga na baadhi ya vifurushi wanavyotoa huduma maalumu za jumbe bila kikomo kwa wateja wao.

Maendeleo

[hariri | hariri chanzo]

Hivi leo, huduma ya ujumbe mfupi umesambaa na kutandaa kote duniani. Kulingana na tovuti ya Forbes, huduma ya jumbe fupi imekuwa ikishamiri kutoka mwaka wa 2019 katika mauzo ya kidijtali hata kuliko matumizi ya barua pepe, Facebook na Twitter. Tovuti ya AXIS inadhihirisha kuwa kati ya wale wote waliotumiwa huduma fupi, asilimia tisini hufungua jumbe hizi ikilinganishwa na asilima ishirini ya waliotumiwa barua pepe.

  1. "What is SMS?". BBC. Iliwekwa mnamo 2009-09-02.
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.