Hifadhi ya Ngorongoro
Hifadhi ya Ngorongoro (kwa Kiingereza: "Ngorongoro Conservation Area") ni hifadhi ya taifa kaskazini mwa Tanzania inayojulikana kote duniani, hasa baada ya kuorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia.
Kiini chake ni eneo la kasoko kubwa lenye umbali wa takriban kilomita 180 kutoka Arusha.
Kuna jumla ya wanyamapori wakubwa takriban 25,000, wakiwa pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pundamilia, nyati, simba, fisi na chui.
Bidii kubwa zaidi ya kulinda wanyama aina ya vifaru zinahitajika haraka kwa sababu idadi ya wanyama hao inazidi kupungua.
Mabaki ya zamadamu katika Olduvai Gorge yanaonyesha kwamba wanyama hao waliokoma walikuweko tangu miaka milioni 3 iliyopita.
Mwaka 1979 Ngorongoro ilipokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO upande wa uasilia.
Katika sekta ya utalii, ambayo nchi kama nchi huitegemea kwa kiasi fulani, ni muhimu serikali iandae miundombinu, hasa barabara zenye ubora wa hali ya juu, ili zitumike kwa muda mrefu na kuboresha sekta nyingine.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Magari ya safari.
-
Makundi ya mifugo ya Wamasai.
-
Ndani ya kreta.
-
Swala na pundamilia.
-
Simba jike akiwa mawindoni.
-
Simba, pundamilia, na swala ndani ya kreta.
-
Makundi ya Wamasai.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya volkeno nchini Tanzania
- Wilaya ya Ngorongoro
- Kasoko ya Ngorongoro
- Orodha ya Urithi wa Dunia katika Afrika
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Ngorongoro Conservation Area Archived 15 Novemba 2008 at the Wayback Machine. at the UNEP World Conservation Monitoring Centre
- Deocampo, D.M., 2004. Hydrogeochemistry in the Ngorongoro Crater, Tanzania, and implications for land use in a World Heritage Site. Applied Geochemistry, volume 19, p. 755-767
- Deocampo, D.M., 2005. Evaporative evolution of surface waters and the role of aqueous CO2 in magnesium silicate precipitation: Lake Eyasi and Ngorongoro Crater, northern Tanzania. South African Journal of Geology, volume 108, p. 493-504.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ngorongoro Conservation Area Authority Archived 23 Juni 2015 at the Wayback Machine.
- Tanzania Tourist Bureau Archived 13 Januari 2010 at the Wayback Machine.
- "UNEP-WCMC World Heritage Site Datasheet" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (pdf) mnamo 2012-09-01. Iliwekwa mnamo 2015-07-09.
- UNESCO World Heritage Site Datasheet
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Ngorongoro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |