[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kilima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vilima.

Kilima ni mwinuko wa ardhi ambao uko juu kuliko eneo linalouzunguka lakini ni mdogo kuliko ule wa mlima. Vilima ni miinuko ya chini kuliko milima. Kwa lugha nyingine ni mlima mdogo, kama Kiswahili kinavyoonyesha wazi. Uso wa kilima ni imara kuliko ile ya tuta la mchanga.

Hakuna ufafanuzi kamili unaokubaliwa kote kuhusu tofauti kati ya kilima na mlima. Katika sehemu za tambarare mwinuko wa mita mia kadhaa unaweza kuitwa "mlima", kinyume chake katika sehemu za milima mirefu mwinuko wa mita 1000 unaweza kuitwa "kilima". Kwa mfano, miinuko ya Ngong karibu na Nairobi huitwa "Ngong Hills" ingawa inafikia kimo cha zaidi ya mita 2,000 juu ya usawa wa bahari. Kwa jumla kilima hutazamwa kuwa kidogo na bila mtelemko mkali kama mlima kamili.

Asili ya vilima mara nyingi ni sawa na asili ya milima; kunjamano ya ganda la Dunia au vilima kama mabaki ya miinuko mirefu zaidi, kwa mfano kutokana na mmomonyoko wa milima mikubwa.