[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Jiolojia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Geology)
Wanajiolojia wakichunguza sampuli za mwamba zilizopatikana kwa njia ya kekee.

Jiolojia (kutoka Kigiriki γῆ ge „ardhi“ na λόγος logos, somo, mafundisho“ = "geologia" - kwa matamshi ya Kiingereza "jiolojia") ni fani ya sayansi inayochunguza maumbile ya dunia na tabia zake za kifizikia na kikemia. Inachungulia pia historia ya dunia na nguvu zinazoendelea kubadilisha maumbile ya dunia.

Neno "geologia" liliwahi kutumiwa mara ya kwanza mnamo 1778 na Mfaransa Jean-André Deluc (17271817).

Jiolojia inatazama mawe na ardhi ikitafuta maelezo kwa umbo na tabia zake kuligana na kanuni za kisayansi.

Kuna masomo madogo ndani ya jiolojia kama vile:

Aina za miamba

[hariri | hariri chanzo]

Jiolojia inachunguza hasa miamba na kutofautisha aina tatu kufuatana na misingi yake:

  • Mwamba Moto: mwamba wa mgando au mwamba wa kivolkeno unajitokeza pale ambako magma au zaha (lava) inaganda.
  • Mwamba Tabaka: mwamba mashapo hutokea pale ambako miamba inavunjika na kusagwa katika mmomonyoko na mashapo yanakandamizwa kwa njia ya kanieneo ya mashapo ya juu hadi mashapo kuwa mwamba mapya.
  • Mwamba Geu: mwamba metamofia ni mageuzi ya miamba ya awali -ama ya kivolkeno au ya mishapo- kwa njia ya kanieneo kubwa sana na joto kali kuwa aina mpya ya mwamba. Metamofosi kwa kawaida hutokea katika kina kubwa.

Asili ya ardhi ni miamba iliyovunjikavunjika na kuchanganyika na mabaki ya mimea na wanyama waliooza.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: