[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Mwamba metamofia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marumaru ni mwamba metamofia uliondwa kutokana na jiwe chokaa kubadilika chini ya shinikizo kubwa kutoka miamba ya juu

Mwamba metamofia (kwa Kiingereza: metamorphic rock) ni aina ya mwamba ambao umebadilishwa na joto kali na shinikizo kubwa. Jina latokana na ing. "metamorphic" iliyochukuliwa kutoka Kigiriki 'morph' (yaani umbo) na 'meta' (yaani badiliko).

Mwamba wa asili unaathiriwa na joto zaidi ya °C 150 hadi 200 na shinikizo la bar 1500). Hii husababisha mabadiliko makubwa katika umbo la mwamba. Mwamba metamofia inaweza kuundwa kutoka mwamba mashapo, mwamba wa mgando au miamba metamofia iliyokuwepo tayari.

Mazingira yenye joto na shinikizo la kutosha yanapatikana katika vilindi chini ya uso wa Dunia. Uzito wa miamba iliyopo juu unasababisha shinikizo, na joto linazidi kuwa juu kadiri tabaka la mwamba lilivyo karibu zaidi na kitovu cha moto cha Dunia. Pale ambapo mabamba ya ganda la Dunia yanasukumana, karibu na chumba cha magma au mlipuko wa volkeno shinikizo na joto ni juu zaidi.

Mifano wa mwamba metamofia ni pamoja na:

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwamba metamofia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.