[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Gameti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Gamete)
Gameti

Gameti (kutoka neno la Kigiriki: γαμετή, gamete, linalohusiana na kitenzi gamein, "kuoa") ni kiini cha kijinsia ambacho kinaungana na kiini cha jinsia nyingine ili kutunga mimba katika viumbehai wanaozaliana.

Gameti hubeba nusu ya habari ya maumbile ya mzazi inayorithishwa kwa mtoto.

Kwa binadamu na baadhi ya wanyama ukubwa wa gameti ni tofauti sana, ile ya kike (ovum, yaani kijiyai) ikiwa mara 100,000 kuliko ile ya kiume (mbegu ya shahawa).

Jina la gameti lilianzishwa na mwanabiolojia wa Austria Gregor Mendel.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gameti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.