Alfabeti
Alfabeti ni kiasi cha alama zinazotumiwa kuandika sauti za lugha fulani. Alama hizi hupatikana kama orodha kwa ufuatano uliokubaliwa, kwa mfano katika Kiswahili: "a, b, ch, d, dh, e, f, g, gh, h, i, j, k, kh, l, m, n, ny, ng', o, p, r, s, sh, u, t, th, v,w, y, z".
Jina la "alfabeti" hutokana na mwandiko wa Kigiriki ambamo herufi mbili za kwanza ni α "alfa" na β "beta".
Alfabeti ni mtindo wa mwandiko uliosambaa duniani kote. Kwa lugha nyingi imechukua nafasi ya miandiko ya awali.
Alfabeti huonyesha sauti si maneno kamili - hii ni tofauti na mwandiko kama Kichina wenye alama kwa ajili ya neno lote.
Mifano ya Alfabeti
[hariri | hariri chanzo]Alfabeti inayotumiwa zaidi kimataifa ni alfabeti ya Kilatini (au "alfabeti ya Kirumi"). Lakini kuna alfabeti nyingine kadhaa zinazojulikana kimataifa kama vile:
- Alfabeti ya Kigiriki hutumiwa kwa lugha ya Kigiriki.
- Alfabeti ya Kiarabu hutumiwa kwa Kiarabu, Kiajemi na Kiurdu.
- Alfabeti ya Kiebrania hutumiwa kwa Kiebrania na Kiyidish.
- Alfabeti ya Kikyrili hutumiwa kwa lugha za Kislavoni kama Kirusi, Kibulgaria, Kiserbia na pia lugha za Asia ya Kati.
Mengine ni alfabeti kama vile ya Kikopti, ya Kigeorgia, ya Kiarmenia n.k.
Aina za pekee za alfabeti ni miandiko ya "abugida". Hii inamaanisha namna ya kuandika ambako hakuna alama za pekee kwa ajili ya vokali. Kila alama ya konsonanti ina namna mbalimbali ya kuonekana kwa kuongeza alama ndogo inayoonyesha ni vokali ipi inayofuata. Mifano yake ni
- Devanagari au alfabeti ya Kihindi
- Alfabeti ya Kiethiopia
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alfabeti kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |