Bara la Antaktiki
Mandhari
Antaktiki ni bara kwenye ncha ya kusini ya dunia. Kwa sababu ya baridi kali katika bara hii, ni bara ya pekee ambapo hawaishi binadamu wowote isipokuwa kuna wanasayansi wanaokaa kwa muda katika vituo vyao. Jina "Antaktiki" latokana na lugha ya Kigiriki likimaanisha "kinyume cha Aktiki" na Aktiki ni eneo karibu na ncha ya kaskazini.
Takriban 98% za eneo la bara lafunikwa na theluji na barafu. Bara liko kati ya bahari za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi. Eneo lake ni kubwa kushinda Ulaya lakini hakuna mti hata mmoja. Bara hili linajulikana kama jangwa
Kuna volkeno hai moja inayotema moto barani ni mlima wa Mount Erebus.
Viungo vya Nje
- Antarctic Place-names Commission of Bulgaria
- L.L. Ivanov et al, Topographic map of Livingston Island and Greenwich Island
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|