Mesite
Mesite | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 2, spishi 3:
|
Mesite (kutoka Kifaransa: mésite) ni ndege wa familia Mesitornithidae. Undugu wa ndege hawa si wa uhakika. Kwa kawaida huainishwa katika Gruiformes, lakini utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kama wana mnasaba zaidi na Columbiformes. Kwa sasa waainishwa katika oda yao yenyewe Mesitornithiformes. Mesite wanafanana na viluwiri wenye miguu na mkia miferu. Rangi yao ni kahawia au kjivu mgongoni na nyeupe au kahawia isioiva chini. Wanatokea Madagaska na hula wadudu, mijusi na vyura wadogo, mbegu na beri. Hulijenga tago lao kwa vijiti katika kichaka na jike huyataga mayai 2-3.
Spishi
hariri- Mesitornis unicolor, Mesite Kahawia (Brown Mesite)
- Mesitornis variegatus, Mesite Kidari-cheupe (White-breasted Mesite)
- Monias benschi, Mesite Domo-mundu (Subdesert Mesite)