[go: up one dir, main page]

Syr Darya (kwa Kigiriki cha Kale ilijulikana kama Ἰαξάρτης, Iaxartes), ni mto wa Asia ya Kati.

Syr Darya
Chanzo Kuungana kwa mito Naryn na Kara Darya katika Bonde la Ferghana
Mdomo Ziwa Aral
Nchi Kirgizia, Uzbekistan, Tajikistan, Kazakhstan
Urefu km 2,212
Kimo cha chanzo m 400
Mkondo m3 1,180 kwa wastani (170 wa chini, 3,900 wa juu)
Eneo la beseni km2
Picha ya mto Syr Darya iliyopigwa kutoka anga-nje.

Chanzo cha maji yake kipo katika Milima ya Tian Shan huko Kirgizia na mashariki mwa Uzbekistan. Mto wenyewe unaanza Kirgizia katika bonde la Ferghana ambako matawimto mikubwa ya Naryn na Kara Darya inaungana. Unaendelea kupita kwa km 2,212 katika Tajikistan, Uzbekistan na Kazakhstan hadi kuishia katika Ziwa Aral.

Pamoja na Amu Darya ni mmoja kati ya mito mikubwa kwenye beseni la Ziwa Aral. Wakati wa utawala wa Umoja wa Kisovyeti maji ya mito hiyo miwili yalitumiwa kwa miradi mikubwa ya umwagiliaji iliyosababisha kukauka kwa asilimia 90 za Ziwa Aral.

Marejeo

hariri

Viungo va Nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Syr Darya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.