[go: up one dir, main page]

Severnaya Zemlya (kwa Kirusi: Северная Земля, yaani Nchi ya kaskazini) ni funguvisiwa la Urusi katika Bahari Aktiki mbele ya pwani ya kaskazini ya Siberia. Inatenganisha bahari za kando za Bahari ya Kara na Bahari ya Laptev.

Visiwa vya Severnaya Zemlya (nyekundu)
Ramani ya Severnaya Zemlya
Severnaya Zemlya kwenye miezi ya barafu

Visiwa vyake huwa na eneo la nchi kavu la km² 37,000. Ni visiwa vinne vikubwa na vingi vidogo.

Severnaya Zemlya ilitambuliwa tu mnamo mwaka 1913, hadi wakati ule haikujulikana. Sababu za kutoijua ni tabianchi yenye baridi kali. Hadi leo hakuna watu wanaoishi huko, sipokuwa wanasayansi wachache kwenye vituo vya utafiti. Bahari inayozunguka visiwa inafunikwa na barafu kwa miezi mingi kila mwaka, hivyo si rahisi kuona mara moja wapi iko theluji juu ya barafu ya bahari na wapi theluji juu ya nchi kavu.

Ramani ya kwanza ilikamilika mnamo 1930-1932.

Visiwa ni sehemu ya mkoa wa Krasnoyarsk Krai.

Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Severnaya Zemlya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.