Kisiwa
(Elekezwa kutoka Visiwa)
Kisiwa ni eneo la nchi kavu kati ya bahari, ziwa au mto linalozungukwa na maji wakati wote. Ukubwa wake hautoshi kukifanya kiitwe "bara".
Visiwa vilivyo karibu kama kundi mara nyingi huitwa "funguvisiwa".
Tofauti kati ya kisiwa kikubwa na bara dogo limeamuliwa kati ya
- Greenland inayoitwa kisiwa kikubwa duniani chenye eneo la kilomita za mraba milioni 2.1 na
- Australia inayotazamwa kuwa bara dogo duniani lenye eneo la kilomita za mraba milioni 7.7.