[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

William Tyndale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
William Tyndale
William Tyndale akifungwa mtini kabla ya kuchomwa motoni baada ya kunyongwa. Mdomoni maneno yake "Lord, ope the King of England's eies"
The Gospell off Sancte Jhon - The fyrst chapter.

William Tyndale alikuwa mwanatheolojia Mwingereza, kasisi ya kanisa na mtaalamu aliyetafsiri Biblia mara ya kwanza katika Kiingereza cha kisasa. Alizaliwa huko Gloucestershire mnamo mwaka 1494 - aliuawa Vilvoorde (Brabant - Ubelgiji ya leo) tarehe 6.9.1536. Tafsiri yake ya Biblia ilikuwa toleo la kwanza lililochapishwa kwa kutumia mitambo mapya ya uchapaji vitabu.

Mawazo yake yalipingwa kwa nguvu zote na watawala na watu wa dini yalionekana kama upinzani wa kidini hivyo aliamua kukimbilia Ujerumani kwa usalama wake, huko alitafuta mchapishaji aliyetoa nakala ya kwanza ya Agano Jipya kwa lugha ya kingereza nakufuatiwa baadaye na agano la kale.

Askofu Kardinali Wolsey alimtangaza kuwa mzushi. Lakini ilikuwa tendo la kupinga ndoa na talaka za mfalme wa Uingereza Henry VIII ilikuwa sababu ya kifo chake. Henry VIII alikasirika juu ya Tyndale akamwomba Kaisari Karl V wa Ujerumani kumkamata. Tyndale alishikwa huko Brussels (mji chini ya Kaisari wakati ule) akasoimamishwa mbele ya mahakama iliyotoa hukumu ya mauti kwa sababu ya uzushi dhidi ya kanisa katoliki. Katika mji wa Vilvoorde penye gereza lake alifungwa mtini akachongwa na mwili wake kuchomwa motoni.