[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Sifongo-bahari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sifongo-bahari
Sifongo kijani (Aplysina aerophoba)
Sifongo kijani (Aplysina aerophoba)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Parazoa
Faila: Porifera
Ngazi za chini

Ngeli 4:

Muundo wa sifongo-bahari; njano: pinakositi, nyekundu: koanositi, kijivu: mesohili, samawati: mtiririko wa maji.

Sifongo-bahari ni wanyama sahili wa maji (bahari na baridi) katika faila Porifera (maana: walio na vinyweleo) ambao wamekazika chini, ijapokuwa spishi chache zinaweza kwenda kwa mbio wa mm 1-4 kwa siku. Spishi nyingi sana zina umbo wa yai, bonge au bomba. Kuna kipenyo kikubwa kiasi juu yao (osculum au kidomo) na vinyweleo vidogo vingi (ostia) kila sehemu ya mwili.

Mwili wa sifongo ni ukuta wa seli tu ambao unazunguka uwazi wa katikati. Ukuta huu umeumbwa kwa tabaka la kolajini (collagen) au mesohili (mesohyl) lililofunikwa na seli nje na ndani. Hata vinyweleo vimezungukwa na seli zinazoitwa porositi (porocytes). Seli zenye kijeledi (flagellum), ambazo huitwa koanositi (choanocytes), zisukuma maji kuelekea osculum na maji mengine yaingia kupitia ostia. Chembe za kulika zilizomo majini ziliwa kwa phagocytosis.

Makala hiyo kuhusu "Sifongo-bahari" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.