[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Shangazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shangazi ni jina ambalo mtoto (wa kiume au wa kike) anamuita ndugu mmojawapo wa familia ambaye anajulikana kama dada wa baba, awe ni mkubwa au mdogo vilevile kwa umri.

Ukilinganisha na lugha za Ulaya, zile za Kibantu zinazingatia zaidi umri na hasa jinsia za wazazi na ndugu zao. Hivyo, neno la Kiingereza "aunt" linaweza kumaanisha "shangazi" (dada wa baba), "mama mkubwa" (kama ni mkubwa wa mama) au "mama mdogo" (kama ni mdogo wa mama). Vilevile anayeitwa kwa Kiingereza "uncle" anaweza akaitwa kwa Kiswahili "mjomba", lakini "baba mkubwa" (kama ni kaka wa baba) au "baba mdogo" (kama ni mdogo wa baba).

Tena kwa Kiingereza "nephew" linaweza kumaanisha "mpwa" lakini pia "mtoto".

Wajibu na haki kati ya shangazi na mtoto wa kaka yake vinategemea utamaduni wa mahali. Katika baadhi ya makabila ana nafasi muhimu katika maamuzi ya ukoo.

Pengine kwa heshima au kwa sababu nyingine mtu anaweza akamuita mwanamke "shangazi" ingawa hawana undugu wowote wa karibu.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shangazi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.