Nyigu-kekeo
Nyigu-kekeo | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Chrysis smaragadula
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Familia 5 zilizo na nyigu-kekeo; jenasi 9 katika Afrika ya Mashariki:
|
Nyigu-kekeo (kutoka kwa Kiing. cuckoo wasps) ni nyigu waliotaga mayai yao katika viota vya nyigu wengine kama kekeo wanavyofanyia ndege wengine. Kuna makundi mbalimbali ya nyigu-kekeo. Familia iliyoenea zaidi na kuwa na spishi nyingi barani Afrika ni Chrysididae yenye spishi 55 katika Afrika ya Mashariki. Jenasi Ceropales ya familia Pompilidae ina spishi 10 za nyigu-kekeo katika Afrika ya Mashariki na kuna spishi 3 katika nusufamilia Bembicinae ya familia Crabronidae. Spishi nyingine za nyigu-kekeo hazitokei Afrika.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Kwa sababu nyigu hawa wako katika makundi mbalimbali ya kitaksonomia, haiwezekani kutoa maelezo ya wao wote pamoja. Tembelea kurasa maalum kwa habari zaidi. Hata hivyo, kwa ujumla, nyigu hawa huwa na kutikulo ngumu kuhimili mashambulizi ya mbuawa wao. Kwa sababu hiyo hiyo, wanaweza kuwa na marekebisho mengine. K.m. spishi za Chrysididae zinaweza kujiviringa katika tufe ili kulinda miguu yao na sehemu za chini za kichwa.
Kama jina lao linavyoonyesha, nyigu hawa wana tabia kama kekeo kwa maana kwamba wao pia hawajengi viota vyao wenyewe, lakini hutaga mayai kwenye viota vya nyigu wengine, kwa kawaida wapweke. Mara nyingi wanadusia spishi moja ya mdusiwa tu au spishi chache.
Spishi za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]
Crabronidae
Chrysididae
|
Pompilidae
|
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Stizoides renicinctus
-
Stilbum cyanurum
-
Trichrysis cyanea
-
Ceropales maculata