[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Lukuledi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Lukuledi)

Kwa maana nyingine ya jina hili angalia Lukuledi (maana)

Mdomo wa mto Lukuledi karibu na Lindi kwenye kiangazi wakati wa maji kupwa

Mto Lukuledi ni kati ya mito ya mkoa wa Lindi (Tanzania Kusini Mashariki) ambayo maji yake yanaingia katika Bahari Hindi kwenye mji wa Lindi.

Mto Lukuledi una urefu wa takriban km 160.

Wakati wa ukame maji si mengi, lakini kwenye km 40 za mwisho kabla ya mdomo maji hupatikana. Kwenye km 20 za mwisho kabla ya mdomo mto hupanuka kuwa hori ya bahari na sehemu hii ya mwisho huitwa pia Lindi Creek.

Bonde la Lukuledi hutenganisha nyanda za juu za Makonde na bonde za juu za Muera.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]