[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Mfumo wa homoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfumo wa homoni

Mfumo wa homoni (kwa Kiingereza endocrine system) ni jumla ya tezi za mwili zinazomwaga homoni kwenye mzunguko wa damu pamoja na ogani zilizo tayari kupokea homoni hizo. Mfumo kwa jumla unaendesha kazi ya ogani za mwili.

Homoni ni kemikali yaani molekuli za pekee zinazowasilisha ujumbe kwa ogani za mwili na kushawishi utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika mwili wa binadamu.

Mfumo kwa jumla unafanywa hasa na tezi za kumwaga homoni katika mzunguko wa damu lakini pia na seli kadhaa za pekee zinazotoa homoni kupitia kuta za seli kwa ogani husika moja kwa moja, kwa mfano kwa moyo, ini, utumbo na nyingine.

Jina la kitaalamu

[hariri | hariri chanzo]

Mfumo wa homoni kwa lugha ya kitaalamu unaitwa "endokrini", yaani "mfumo unaomwaga ndani" kwa maana ya ndani ya mzunguko wa damu. Hii ni tofauti na tezi "exokrini" ("kumwaga nje") zinazotoa homoni au kiowevu cha pekee nje yake kupitia kichirizi hadi pale kinapotakiwa, kwa mfano tezi za jasho (kwenda ngozi ya nje).

Utaalamu wa mfumo wa homoni huitwa "endocrinology" ambayo ni tawi la elimu ya tiba ya ndani. Mfumo wote husimamiwa na kuongozwa na sehemu ya ubongo inayoitwa hypothalamus.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mfumo wa homoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.