Margaret Baba Diri
Margaret Baba Diri | |
Amezaliwa | 1954 Uganda |
---|---|
Nchi | Uganda |
Kazi yake | siasa |
Margaret Baba Diri (alizaliwa 29 Juni 1954) ni mwanasiasa wa Uganda ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza kwenye Bunge la Uganda kama mwakilishi wa watu wenye ulemavu mwaka 1996 ambako amedumu hadi sasa.
Kabla ya kujiunga na siasa alifanya kazi kama mwalimu kwenye shule ya St. Charles Lwanga huko Koboko kati ya 1976 na 1990 na pia kama afisa wa maendeleo ya jinsia kwenye Umoja wa Kitaifa wa Watu Walemavu wa Uganda (NUDIPU) Archived 25 Februari 2022 at the Wayback Machine. kati ya 1992 na 1996. [1]
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Margaret Baba Diri ana Diploma ya Elimu kutoka Chuo cha Taifa cha Ualimu Kyambogo, pia alipata Shahada ya Kwanza ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Kyambogo [2]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Margaret Baba Diri alianza taaluma yake kama mwalimu shule ya St. Charles Lwanga Koboko kati ya mwaka 1976 na 1990 na kama afisa wa maendeleo ya jinsia kwenye Muungano wa Kitaifa wa Watu Walemavu wa Uganda (NUDIPU) kati ya 1992 na 1996. [3]
Baadaye alijiunga na siasa kama mwakilishi wa watu wenye ulemavu bungeni. Amekuwa Bungeni kwa vipindi vitano kuanzia mwaka 1996 ambapo pia alimwakilisha Koboko kama Mbunge Mwanamke. [4] Margaret Baba Diri ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Tume ya Mamlaka za Serikali na Biashara pia mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Elimu na Michezo [5]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Margaret Baba Diri ni mjane. [6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Baba Diri Margaret". Parliament of Uganda. parliament of uganda. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-27. Iliwekwa mnamo 15 Aprili 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Baba Diri Margaret". Parliament of Uganda. parliament of uganda. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-27. Iliwekwa mnamo 15 Aprili 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Baba Diri Margaret" Archived 27 Aprili 2021 at the Wayback Machine.. Parliament of Uganda. - ↑ "Baba Diri Margaret". Parliament of Uganda. parliament of uganda. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-27. Iliwekwa mnamo 15 Aprili 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Baba Diri Margaret" Archived 27 Aprili 2021 at the Wayback Machine.. Parliament of Uganda. - ↑ "Visually impaired MP, Margaret Baba Diri still striving in Parliament".
- ↑ "Baba Diri Margaret". Iliwekwa mnamo 15 Aprili 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Baba Diri Margaret". Iliwekwa mnamo 15 Aprili 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Baba Diri Margaret"
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Margaret Baba Diri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |