[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Mankala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aina ya bao mmoja ya kucheza mankala.
Bao mmoja ya kucheza aina ya mankala Toguz korgool en bois.
Sanamu ya watu wakicheza mankala.

Mankala ni jina la kimataifa kwa michezo inayofanana na bao. Ni kundi la michezo kwa wachezaji wawili wanaohamisha kete (vijiwe, mbegu) kati ya nafasi zilizopangwa, mara nyingi mashimo katika bodi ya bao, ardhini au katika jiwe.

Michezo ya mankala inachezwa mahali pengi duniani. Inapendwa sana Afrika na Asia. Michezo hizi, zilitoka Africa.[1]

Kwa kawaida, watu wawili wanacheza. Wanaweka kete ndani ya shimo. Mchezaji mmoja anachagua shimo, anatoa kete, na anaziweka kwa shimo zingine moja kwa moja. Wachezaji wanajaribu kupata kete nyingi zaidi ili washinde. Lakina, kuna aina nyingi na kanuni tofauti za kukamata kete na kuziweka kwa shimo. Pia, michezo hizi za aina ya mankala zina idadi ya shimo tofauti. Lakini michezo hii yote ni michezo ya akili, na inasomesha watu kufanya hesabu. Kwa hivyo, watu wanapenda kuwafundisha watoto wao kucheza.

Jina la Mankala

[hariri | hariri chanzo]

Jina la Mankala linatumikakwa aina ya michezo tofauti, na kwa familia ya michezo. Jina hili ni la Kiarabu (منقلة), na linafanana na naqala (نقلة), yaani kuendelea.[2][3][4]

Soma pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Meyers, Eric M.; Research, American Schools of Oriental (Februari 7, 1997). The Oxford Encyclopedia of Archaeology in the Near East. Oxford University Press. ISBN 9780195112160 – kutoka Google Books.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "English words from Arabic". zompist. Iliwekwa mnamo 2015-12-03.
  3. "Mancala". Lexbook. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-12-08. Iliwekwa mnamo 2015-12-03. {{cite web}}: More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)
  4. Cannon, Garland; Kaye, Alan S. (1994). The Arabic contributions to the English language : an historical dictionary. Wiesbaden: Harrassowitz. uk. 81. ISBN 3-447-03491-2. Iliwekwa mnamo 2015-12-03.