[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Mzunguko

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mzunguko

[hariri chanzo]

Hii si tafsiri sahihi ya ORBIT. Tukisema MZUNGUKO tupu bila sababu tutakuwa tunapotosha watu wanaotufuatilia. Njiamzingo ni neno sahihi walilopitisha na kamusi ya KAST. Hebu soma hapa:

obiti (orbit): njia ya elektroni kuzunguka nyukilia (kiini) ya atorni. Njia hizo ziko katika ngazi tofauti za viwango vya nishati. Pia: njiamzingo

Ikiwa kutakuwa na majadiliano kabla ya kubadili maumbo ya majina ya makala hizi itakuwa vema sana. Maana tulishiriki mjadala huu katika Chuo Kiku Huria mwaka 2018. Hadi kamusi iliundwa. Sasa kutakuwa na mambo tofauti jinsi inavyoenda. MuddybLonga 04:09, 5 Oktoba 2024 (UTC)[jibu]

Shida ni hiyohiyo, mwenzetu anajiamini sana kubadilisha anavyoona bila kushauriana kwanza. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:12, 5 Oktoba 2024 (UTC)[jibu]
Badiliko hilo ni la miezi 5 iliyopita...
Hata hivyo, KAST si sanifu. Kwa mujibu wa TUKI tafsiri sanifu ndiyo "mzunguko". Sina kamusi sasa hivi lakini kwa kumbukumbu yangu tafsiri hiyo iko kwenye "Kamusi sanifu ya biolojia, fizikia, na kemia" na kamusi zenginezo za TUKI.
Pia tunasema "dunia huzunguka jua", hivyo kwa maoni yangu ni wazi kueleza tendo hilo kama "mzunguko." Tukisema "njiamzingo" inaanza kuwa ngumu kutafsiri "orbit" kama kitenzi, kwa mfano: "the earth orbits the sun." tungetafsiri vipi? Nadhani ni wazi na ekevu zaidi kutafsiri kwa namna sawa katika hali zote mbili, yaani: "the earth orbits the sun => dunia huzunguka jua" "the earth's orbit => mzunguko wa dunia".
Zaidi ya hayo, nimeona mara nyingi "mzunguko wa dunia, mwezi huzunguka dunia" n.k. lakini "njiamzingo" ni adimu sana.
Tunaweza kuweka "njiamzingo" kama tafsiri nyingine lakini kwa kweli nadhani ni bora kuweka "mzunguko" kama jina kuu la makala, kwa sababu ndiyo tafsiri sanifu na kawaida zaidi. Kisare (majadiliano) 02:37, 14 Oktoba 2024 (UTC)[jibu]
Hata hivyo, kwangu si muhimu kujadiliana/kupigana sana kuhusu suala hilo Kisare (majadiliano) 02:54, 14 Oktoba 2024 (UTC)[jibu]
Kupigana tena? Tunajadiliana kama inavyotaka Wikipedia kujadiliana katika masuala mtambuka. KAST ni sanifu. Kwa sababu ilitolewa na serikali. Si kwamba mtu alipanga. Pia tutofautishe kati ya jina na tendo. Pia, tukiwa tunajadiliana si vema kuonyeshana umwamba. Hatujengi tunabomoa. Kitu ambacho si sawa. MuddybLonga 15:49, 14 Oktoba 2024 (UTC)[jibu]
Sijaribu "kuonyeshana umwamba". Kwa kweli sitaki kupigana.
KAST haikuchapishwa na TUKI. Iliandikwa na baadhi ya wataalamu wa UDSM, ikachapishwa na "Ben & Company Limited". Kwa hiyo nilisema si "sanifu", kwa sababu si chapisho la TUKI. Naamini ni bora tufuate pendekezo la TUKI.
Kwa maoni yangu, tendo na jina vinafaa kufanana. Yaani, hivyo ndivyo ilivyo katika lugha zengine. Kwa mfano, kwa Kiingereza nomino ni "orbit" na kitenzi ni "orbit". Kwa Kihispania, nomino ni "órbita" na kitenzi ni "orbitar". Kwa Kizulu, nomino ni "uzungezo/uzungezohlelo" (inayofanana na Kiswahili) na kitenzi ni "zungeza". Kisare (majadiliano) 20:13, 21 Oktoba 2024 (UTC)[jibu]