James Stafford
Mandhari
James Francis Stafford (alizaliwa 26 Julai 1932) ni Kardinali wa Kanisa Katoliki kutoka Marekani. Alihudumu kama msimamizi mkuu wa Idara ya Upatanisho wa Kitume kutoka mwaka 2003 hadi 2009.[1]
Kabla ya kushika wadhifa huo, Stafford aliwahi kuhudumu kama raisi wa Baraza la Kipapa la Walei (1996–2003), askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Denver (1986–1996), askofu wa Jimbo la Memphis (1982–1986), na askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Baltimore (1976–1982). [2]Alipewa hadhi ya kadinali na Papa John Paul II mwaka 1998.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Stafford card. James Francis", Holy See.
- ↑ Kigezo:Catholic-hierarchy
- ↑ Miranda, Salvador. "STAFFORD, James Francis (1932– )", The Cardinals of the Holy Roman Church. Retrieved on 2024-10-08. Archived from the original on 2014-01-04.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |