[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Hariri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vifukofuko vya hariri ilhali viwawi wako bado ndani
Wakinamama wafungua nyuzi kwa kupiga vifukofuko vya hariri baada ya kuchemshwa (picha ya China karne ya 12)
Mama atoa nyuzi za hariri kutoka vifungu vilivyochemshwa

Hariri ni uzi asilia inayopatikana kutoka kwa kifukofuko cha kivawi cha nondo-hariri wa Asia, Bombyx mori, au nondo wengine, kama nondo-hariri wa Afrika, Gonometa postica, au Anaphe panda wa Msitu wa Kakamega, Kenya. Nyuzi zake zatumiwa kwa kutengeneza kitambaa.

Kihistoria watu wa China walikuwa wa kwanza wenye ujuzi wa kutengeneza hariri. Kitambaa cha hariri kilipelekwa kote Asia na Ulaya kupitia barabara ya hariri na kuuzwa kwa bei kubwa.

Wachina walifaulu kwa karne nyingi kuficha siri ya hariri. Mwaka 555 wamonaki Wakristo walifaulu kubeba mayai ya kipopo hadi Bizanti na kuyampatia Kaisari wa Dola la Roma ya Mashariki. Tangu siku zile hariri ilitengenezwa pia katika nchi za Mediteranea.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hariri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.