Kuzimu
Mandhari
Kuzimu ni huko ambako binadamu wanasadikiwa kuendelea kuishi baada ya kufariki dunia.
Imani hiyo ni ya zamani sana na kujitokeza katika visasili na dini nyingi, kuanzia dini za jadi.
Ingawa imani hiyo ina tofauti nyingi, kwa jumla wengi wanasadiki mtu (au roho yake) anaendelea kuishi kama mzimu.
Katika Biblia kuna maendeleo ya ufunuo hata kuhusu suala la kuzimu, na ukamilifu wake uliletwa na Yesu ambaye alifundisha ufufuko wa wafu na uzima wa milele, lakini pia anasadikiwa kuwa kisha kufa alishukia kuzimu ili kutoa huko waadilifu wa kale kwa kuwatenganisha moja kwa moja na waovu na kuwaleta pamoja naye mbinguni.
Tanbihi
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |