[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kichoma-mguu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kichoma-mguu
Vichoma-mguu ikimea kando ya njia
Vichoma-mguu ikimea kando ya njia
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama jaja)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Manyasi)
Nusufamilia: Panicoideae
Jenasi: Heteropogon
Spishi: H. contortus
(L.) Roem. & Schult.

Kichoma-mguu, kichoma-nguo au kishona-nguo (Heteropogon contortus) ni spishi ya nyasi katika nusufamilia Panicoideae. Lakini majina haya hutumika vilevile kueleza mmea mwingine: Bidens pilosa, gugu baya shambani. H. contortus inatokea kanda za tropiki za Afrika, Asia ya Kusini, kaskazini kwa Australia na Oceania. Imesamba katika kanda za tropiki na nusutropiki za Asia ya Mashariki na imewasilishwa pia katika Amerika. Nyasi hili hukua katika vishungi na linaweza kufika m 1.5. Mbegu ina unywele mrefu upande mmoja na ncha kali upande mwingine. Unywele huwa songosongo ukiwa mkavu na mnyofu ukiwa umefyonza maji. Mizunguko ya ukavu na unyevu inayorudiwa inasukuma mbegu ndani ya udongo. Lakini kama mbegu ikiingia kwenye manyoya ya mnyama, inaweza kusukumwa katika ngozi na kuuma mnyama.

Katika nchi nyingi watu wanapenda kutumia kichoma-mguu kwa kuvimba mapaa. Likiwa changa nyasi hili ni lishe nzuri kwa wanyama wafugwao, lakini likitoa mbegu kuingia kwa machungani kwenye nyasi hili ni hatari kwa wanyama, na hata kwa watu. Mbegu huingia kwa manyoya au kwa nguo na kudunga ngozi.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]