[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kibera (Nairobi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kibera mwaka 2020.

Kibera ni mtaa katika jiji la Nairobi, mji mkuu wa Kenya ambapo watu huishi na kufanya kazi ndogo ndogo kama kuuza mahindi ya kushemshwa,matunda, mboga na kadhalika. Baadhi ya watu hao, kunao ambao hawawezi kufanya kazi yoyote. Hata hivyo, watu wengi wameonyesha sifa mbaya dhidi ya mtaa huo wa Kibera lakini, tunafaa kukumbuka ya kwamba kila kitu kina uzuri wake.

Vile vile tunaweza kuwa na nia njema kuhusu mitaa kama hiii ili tusiwe kama watu ambao wanasema lakini kufanya ni shida sana. Isitoshe sio kupenda kwa wale walioko kwenye hii jinamizi la umaskini, lakini ni sababu chache zilizowaelekeza kwenye hili dimbwi la umaskini.

Watu wengi katika mtaa wa kibera huwa wanafanya kazi mbali mbali ili kujimudu kimaisha. Baadhi ya kazi wanazozifanya ni kama uchuuzi,kuosha nguo za majirani ili kuwawezesha kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine. Kuna wale ambao hawana namna ya kuwawezesha kufanya kazi yoyote maishani. Ajira ni kikwazo kikubwa kwa wakaazi wa kibera. Umaskini ni jambo la kuzingatiwa katika mtaa wa kibera kwa maana ndio mojawapo ya shida ambazo zinawakumba wenyeji.

Takriban ya watu nusu milioni kwenye mitaa wa mabanda wa kibera wamekuwa kwenya mstari wa mbele kuimarisha maisha ya wanachi wanaoishi katika mitaa ya mabanda kuwa ya kawaida na ya kuaminika na wageni kutoka nchi za ng'ambo.

Ingawa kuna shida ya mavazi, chakula lakini ajira imechangia sana kueneza umaskini katika jamii ya mitaa wa Kibera. Hii ni kwasababu, upande wa ajira watu wengi hawana mtaji wa kuanzisha biashara ndogo ndogo ili kuwawezesha kuishi maisha ya kawaida.

Kwa hakika umaskini sio jambo la kujitakia bali ni jambo ambalo linaweza kukumba mtu yeyote.Isitoshe, tunafaa kuwa na nia njema kuhusu mtaa wetu wa Kibera na kutafuta njia ambazo zinaweza kulikabili janga hili la umaskini.Pia, tunafaa kuwaamusha walio kwenye jinamzi la umaskini kuwa litatokomea kulingana na bidii yetu.Kwani wahenga hawakutupaka mafuta ya samaki kwenye mgongo wa chupa walipolonga kuwa "Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu."

Uharibifu wa mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Kwanza, kuwepo kwa mazingira duni mahali popte tunapokaa hudhuru kiazya kwa kuleta maradhi milini yetu kwa hivyo ni jukumu letu kama binadamu tuzingatie vikwazo kamili ili tuweze kuboresha hali ya maisha yetu na kujikinga dhidi ya maambukizo yanayotokana na mazingira duni.

Kitongoji duni cha Kibera pekee kinayo idadi ya takribani watu milioni mbili, ukilinganisha na nafasi ya ardhi iliepo, hii ni idadi kubwa sana. Hii inaleta ukosefu wa mpangilio mwafaka katika ujenzi wa maeneo ya makazi. Mpangilio huu duni ndio kiini cha ukosefu wa mazingira bora na pia kuchangia katika uenezaji wa maradhi.

Mpangilio huu duni vile vile huleta madhara yafuatayo:

  • Hakuna vyumba vya kutosha vya wakaaji wa Kibera, kwa sababu ni chache ukilinganisha na idadi ya watu.
  • Hakuna nafasi ya kujenga vyumba vipya na kutokana na kuwepo na nafasi ya kujenga watu huwa na shida ya kutokuwa na vioo. Wengi huenda haja zao wakati giza imeingia halafu wanarusha nnje hwa njia isiyofaa kwa kutojali wanarusha wapi.
  • Hakuna pahali pametengwa pa kutupa takataka. Katika mazingira mwa Kibera kumechacha mithili ya siafu kwa chembe chembe ya sukari. Aidha, kuna ukosefu wa bwawa la maji taka. Na kama kunayo vimevunjika ndiyo husababisha maaradhi mengi kama: kipindupindu, malaria, kuendesha, kusokotwa na tumbo na mengineo.

Kwa mukhtasari ijapokuwa maisha kwenye kitongoji duni kumekera kwa hao, wakaaji wanaofaa kuzingatia usafi kwa kila wawezavyo ili kumarika mazingira.

Picha za Kibera

[hariri | hariri chanzo]