[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kasese

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kasese
Kasese is located in Uganda
Kasese
Kasese

Mahali pa mji wa Kasese katika Uganda

Majiranukta: 0°11′12″N 30°05′17″E / 0.18667°N 30.08806°E / 0.18667; 30.08806
Nchi Uganda
Mkoa Magharibi
Wilaya Kasese
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 66,600
Mji wa Kasese

Kasese ni mji mkuu wa Wilaya ya Kasese nchini Uganda wenye wakazi wake takribani 66,600. Mji uko magharibi mwa Ziwa George. Awali mji huu ulikua kutokana na uchimbaji wa madini ya shaba katika eneo ka Kilembe, na hapo baadaye uchimbaji wa kobalti. Huu ndio mji mkuu wa Wilaya ya Kasese na makao makuu ya wilaya yapo hapo. Kasese pia ndio mji mkubwa kwenye Mkoa wa Rwenzururu. Makazi ya Charles Mumbere, Omusinga wa Rwenzururu yako katika mji huu.

Kasese ni mji ulioko sehemu ya mwisho kabisa ya Reli ya Uganda upande wa magharibi inyoelekea Kampala na Tororo na pia ndipo ulipo Uwanja wa Ndege wa Kasese. Mji uko jirani na Milima ya Rwenzori na Mbuga ya Kitaifa ya Queen Elizabeth.

Idadi ya wakazɪ

[hariri | hariri chanzo]
Old Kituo cha garimoshi Kasese

Agosti 2014, Uganda Bureau of Statistics ilikaridia kuwa Kasese ina wakazi wapatao 101,679.[1] Kasese ni kati ya miji inayokua kwa kasi zaidi nchini Uganda.

Mgodi wa uchimbaji wa shaba wa Kilembe

Vivutio hivi vimo katika mji huu na pembezoni mwake:

  • Makao makuu ya Wilaya ya Kasese
  • Ofisi za halmashauri ya Kasese
  • Soko kuu la Kasese
  • Hima Cement Limited
  • Uwanja wa ndege wa Kasese
  • Mgodi wa uchimbaji wa shaba Kilembe

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. UBOS (27 Agosti 2014). "The Population of The Regions of the Republic of Uganda And All Cities And Towns of More Than 15,000 Inhabitants". Citypopulation.de Quoting Uganda Bureau of Statistics (UBOS). Iliwekwa mnamo 22 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kasese travel guide kutoka Wikisafiri