[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kadi karadha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa uso wa kadi karadha:
1. Logo ya benki iliyotoa kadi
2. Chipu (kwenye "kadi janja")
3. Alama ya usalama (hologramu)
4. Namba ya kadi
5. Logo ya kadi
6. Tarehe ya kumalizika kwa kadi
7. Jina la mwenye kadi
8. Chipu


Kadi karadha (au Kadi ya mkopo (kwa Kiingereza: credit card) ni kadi ya kulipia iliyotolewa kwa watumiaji (wamiliki wa kadi) ili kuwawezesha kulipa mfanyabiashara kwa bidhaa na huduma.

Mtoaji wa kadi (kawaida huwa ni benki) anatoa mikopo kwa mmiliki wa kadi ambaye hulipa benki baadaye. Malipo yake hujumuisha riba.

Mkabidhi kadi (benki) huunda akaunti mzunguko na kumpa mmliki kadi mikopo ainati ambayo mwenye kadi anaweza kukopa fedha za kulipia ununuzi au fedha anazozihitaji.

Kwa maneno mengine, kadi ya mkopo hujumlisha kufanya malipo pamoja na mikopo zaidi.

Miundo tata ya anda katika viwanda vya kadi ya mkopo yaweza kumzuia mteja uwezo wa kulinganisha maduka, hii ni njia ya kuhakikisha kuwa viwanda hivi havina mashindano ya bei hivyo kupata faida iliyo juu.

Kutokana na wasiwasi wa shughuli kama hizo, sheria nyingi zimetumika kudhibiti malipo ya kadi za mkopo.

Kadi ya mkopo ni tofauti na kadi ya kulipa (charge card) ambayo huhitaji kulipa matumizi yote kwa ukamilifu baada ya mwezi, kinyume na kadi ya mkopo unaomwezesha mtumizi kuendeleza deni kulingana na riba anayotozwa juu yake.

Kadi ya mkopo pia ni tofauti na kadi ya fedha (cash card) ambayo inaweza kutumiwa na mwenye kadi kama sarafu.

Kadi ya mkopo pia ni tofauti na kadi ya malipo kwa kuwa kadi ya mkopo inahusisha mhusika wa tatu (benki) anayelipa muuzaji na baadaye anarejeshewa fedha hizo na mnunuzi, ilhali kadi ya malipo mnunuzi huchelewesha tu malipo hadi siku nyingine.

Historia ya kadi ya mikopo

[hariri | hariri chanzo]

Dhana ya kutumia kadi kufanyia malipo ilielezewa mwaka 1887 na Edward Bellamy katika novela yake Looking Backwards. Bellamy alitumia msamiati ‘kadi ya mkopo’ mara kumi na moja kwa novela hii ilhali alikuwa akirejelea kadi iliyotumika na wananchi kutumia pesa walizopewa na serikali pasipo kukopa, hivyo kufanya sawa na kadi ya debit.

Wizi wa kadi za mikopo

[hariri | hariri chanzo]

Hatari kuu katika utumizi wa kadi ya mikopo ni wizi wa kadi yenyewe au maandishi yaliyomo kama vile jina, nambari ya akaunti ya benki na anwani yako. Wanaotumia kadi hizi huombwa kuwa makini zisije zikaibwa wakajikuta wameporwa pesa zao au kadi zao zikafanya manunuzi na mikopo bila ya wao kujua. Wizi huu hujulikana kama identity theft. Kuukwepa wafaa kujulisha kampuni iliyokupa kadi mara moja baada ya kuibiwa kadi. Wafaa pia uweke kadi yako mahala pema ambapo haitaporwa[1].

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kadi karadha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.