[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Kondomu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kondomu iliyokunjwa
Kondomu iliyokunjuliwa
Kondomu kwa mwanamke

Kondomu ni kifuko kinachotumiwa na wanaume tangu zamani kuzuia mimba na maambukizi ya maradhi ya zinaa kama vile UKIMWI. Siku hizi kuna kondomu ya kike pia.

Utengenezaji

[hariri | hariri chanzo]

Kondomu zinatengenezwa kwa ngozi ya mnyama au siku hizi zaidi kwa kutumia mpira.

Utengenezaji hufanyika katika mazingira ya baridi ili kuhifadhi uimara wa mpira.

Zinaunganishwa ngozi nyembamba mbili ili matundu ya ngozi ya kwanza yazibwe na ile ya pili na matundu ya ngozi ya pili yazibwe na ile ya kwanza.

Kisha kupimwa, kondomu huwekewa dawa ya kuzuia isiharibike: dawa hiyo ina madhara kwa afya.

Kondomu zinapofungwa katika visanduku, hivyo hubandikwa karatasi zinazomueleza mtumiaji kuwa asitegemee sana kondomu kama kinga dhidi ya Ukimwi. Lakini iwapo vitauzwa katika nchi maskini angalisho hilo halibandikwi; pengine badala yake vitaandikwa kwamba kondomu ni kinga kamili, imara au madhubuti.

Uchukuzi

[hariri | hariri chanzo]

Visanduku vikitolewa kiwandani kwenye baridi hupakiwa hadi melini na kuanza safari ya miezi baharini vikikumbana na joto kali (hata 70°C) ndani ya kontena.

Pengine vinabaki humohumo muda mrefu hata katika bandari (kwa mfano: Tanga au Dar es Salaam nchini Tanzania) mpaka viruhusiwe kutolewa.

Joto la huko linazidi kuathiri uimara wa mpira, hata pengine linafanya uanze kuyeyuka.

Matatizo katika matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Mara nyingi kondomu inashindwa kazi na kuruhusu maambukizi kwa sababu:

1. Ina vitundu vidogovidogo kama aina zote za mpira. Ukubwa wa vitundu hivyo ukipimwa: ni mikron 5, wakati ukubwa wa virusi ya Ukimwi (HIV) ni mikron 0.1 tu, yaani kila kitundu ni kikubwa mara 50 kuliko virusi.

2. Wakati wa kuitumia kuna nguvu ya msukumo au mkandamizo, mpishano wa ngozi zake mbili, msuguano wa mpira kati ya watu wawili. Matokeo ni kondomu kuchunika na hatimaye kulika kwa sababu dawa ya kuihifadhi inachanganyikana na tindikali za uke.

3. Pengine kondomu wakati wa ngono hutoka au kupasuka.

Pamoja na hayo:

4. Ingebidi kufuata kanuni kumi za namna sahihi ya kutumia kondomu. Hii inamhangaisha mwanamume kuifikiria sana wakati wa ngono, ikizuia umoja wake na mwenzake na kupunguza raha ya wote wawili. Kutofikia msisimko kunamtesa sana mwanamke moyoni.

5. Wanawake wengine badala ya furaha wanapatwa na maumivu kwa sababu ya msuguano kati ya kondomu na ukuta laini wa uke. Matokeo yake ni ukuta huo kutokwa daima na aina ya majimaji.

Mafanikio

[hariri | hariri chanzo]

Pamoja na kutumika kwa ajili ya kuzuia mimba kwa mafanikio makubwa (ingawa si 100%), mpira huo unatangazwa sana kama kinga imara dhidi ya virusi vya ukimwi.

Lakini katika utafiti uliofanywa na shirika la Sexuality Information and Education Council la Marekani kwa majozi 122 ambapo mmojawao alikuwa mwathirika, wenzao 12 waliambukizwa (10%) ingawa walifanya ngono kwa kutumia kondomu kila mara na kwa usahihi.

Shirika la Human Life International lilifanya utafiti kwa aina mbalimbali za ngono. Kati ya waliotumia vizuri kondomu, mwaka wa kwanza waliambukizwa: 11% za waliofanya ngono ya kawaida, 30% za waliofanya ulawiti. Mwaka wa pili wakafikia 21% na 51%. Mwaka wa tatu wakawa 30% na 66%.

Kwa maneno mengine ni kwamba kondomu haizuii moja kwa moja, bali inaahirisha maambukizi: kama si leo, inaweza kuwa kesho.

Katika mapambano dhidi ya UKimwi, shida kubwa ni kwamba matangazo mengi yanapotosha kwa kumtumainisha mteja kwamba kondomu ni salama kabisa, hivyo anaweza akaendelea na ngono bila wasiwasi.

Matokeo ni kwamba anaweza akaambukizwa, halafu akaambukiza wengine akidhani ni salama.

Angejua ukweli huo pengine angekwepa ngono ili kulinda uhai wake na wa wengine.

Mtazamo wa maadili

[hariri | hariri chanzo]
Kondomu nyingi baada ya kutumika zunatupwa popote, hata barabarani kama hii. Pengine watoto wanaziokota na kuzitumia kama vipulizo.

Wapo wanaopinga matumizi ya kondomu hata kwa hoja za maadili kama ifuatavyo.

Lengo la kuzuia vijidudu visilete maradhi na hatimaye kifo ni zuri; vilevile pengine familia inahitaji kupanga uzazi.

Hata hivyo lengo jema halihalalishi njia mbaya mbele ya Mungu.

Ni muhimu kuchagua njia ya kufaa pande zote, na kuchunguza ukweli wa maneno ya wanaohimiza kutumia kondomu.

Kondomu inavuruga utaratibu, maana, thamani na heshima ya ndoa ikiingilia kiini chake kwa kuzuia umoja wa miili ya mume na mke: badala ya tendo la ndoa kuna watu wawili wanaosugua mpira kwa viungo vya uzazi; uwezekano wa kuzaa mtoto unapungua sana.

Dhambi hiyo ni kubwa zaidi ikifanywa nje ya ndoa: kwa vyovyote inawatenganisha wote wawili na Mungu badala ya kuwaunganisha naye katika kuendeleza uumbaji.

Uhamasishaji wa matumizi ya kondomu unaua dhamiri za watu waone ubaya katika maradhi na mimba wasione uovu wa dhambi wala matokeo yake ya kiroho, hasa ikitumika nje ya ndoa au kabla ya ndoa.

Kwa mtazamo huo, mtetezi na msambazaji wa kondomu anatenda hasa dhambi za: 1. kudanganya kibiashara (kutapeli kwamba ni kinga imara, wakati si hivyo); 2. kumsaidia jirani kuzini au walau kuzuia vibaya uzazi katika ndoa; 3. kusababisha kifo cha watu wengi watakaoambukizwa hata baada ya miaka kutokana na baadhi ya kondomu kufeli.

Wengine wanalaumu kondomu, hasa za plastiki, kwa kuchafua mazingira.