[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Chuma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Feri (chuma))


Chuma (Feri)
Jina la Elementi Chuma (Feri)
Alama Fe
Namba atomia 26
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 55.845
Valensi 2, 8, 14, 2
Ugumu (Mohs) 4
Kiwango cha kuyeyuka 1811 K (1538 °C)
Kiwango cha kuchemka 3134 K (2861 °C)
Asilimia za ganda la dunia 4.7 %
Hali maada mango

Chuma (kisayansi pia: feri kutoka Kilatini "ferrum"; kifupi: Fe) ni elementi na metali inayopatikana kwa wingi duniani. Kikemia ni elementi mpito yenye namba atomia 26 katika mfumo radidia.

Chuma ni kati ya metali muhimu sana duniani. Chuma ni msingi wa feleji (chuma cha pua) ambayo ni uti wa mgongo wa maendeleo ya kiteknolojia ya miaka 100 iliyopita. Asilimia 95 ya vifaa vote vya metali vinavyotengenezwa duniani ni chuma.

Udhaifu wa chuma kwa matumizi yake ni tabia yake ya kubadilika kuwa kutu.

Madini chuma ni muhimu sana katika mwili wa binadamu na wanyama. Upungufu wake ni wa kawaida sana duniani na unasababisha maradhi mbalimbali kuanzia upungufu wa wekundu wa damu na hatimaye wa damu yenyewe. Kwa mfano nchini Tanzania asilimia 58 za watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wana upungufu huo [1].

Utatuzi wa tatizo hilo ni kula vitu vyenye chuma kwa wingi kama nyama za ndani (ini, figo, moyo), dagaa na samaki wengine, lakini pia mboga kama matembele, mnavu, mchicha, kisamvu na mlenda.

Kula matunda yenye uchachu kama vile machungwa, ubuyu na ukwaju pamoja na vitu hivyo kunarahisisha ufyonzwaji wa madini chuma. Ni kinyume chake kwa unywaji wa chai na kahawa wakati wa mlo.

Picha

Tanbihi

  1. TDHS 2015/2016

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuma kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.